Waziri wa Ujenzi Dkt. John Pombe Magufuli (Mb) amemtaka Mkandarasi wa Kampuni ya J.V anayejenga barabara ya Makutano-Nyamuswa - Ikoma Gate, sehemu ya (Makutano-Natta km50) kufanya kazi usiku na mchana ili kukamilisha mradi huo kwa wakati.
Waziri Magufuli alitoa tamko hilo jana wakati akihutubia mamia ya wakazi wa mji Butiama mkoani Mara.
“Najua bado mnaidai serikali zaidi ya shilingi bilioni tatu lakini hii isiwe sababu ya kushindwa kuendelea na kazi japo mlishaonyesha mfano mzuri wa kuanza kujenga daraja la Kyarano” alisema Waziri Magufuli
Aidha, Waziri Magufuli aliahidi kuwa ndani ya wiki mbili atatafuta fedha kwa ajili ya kumlipa Mkandarasi huyo ili aweze kuendelea na kazi kwa kasi kubwa.
“Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Barabara yupo hapa pamoja na wataalamu wangu, tutahakikisha ndani ya wiki mbili tutatafuta fedha kwa ajili ya kumlipa Mkandarasi pamoja na fidia na kuondoa nguzo za umeme” Aligusia Waziri Magufuli
Pia Waziri Magufuli aliwatoa hofu Wananchi wa Butiama kwa kusema kuwa wale wote waliofuatwa na barabara katika maeneo yao watafidiwa kama sheria inavyoeleza.
“Nawahakikishia kuwa wale wote mliofuatwa na barabara hii mtafidiwa kwa mujibu wa sheria, ila kwa wale wote walioifata barabara wabomoe wenyewe nyumba zao”
Aidha, Waziri Magufuli amepinga wazo la Halmashauri ya Wilaya ya Butiama kutaka kumtoza fedha Mkandarasi wa Kichina kwa ajili ya mawe anayotumia kujengea barabara mkoani Mara.
“Hapa sikubaliani na wazo lenu yaani Mkandarasi anachukua mawe anapasua kokoto kwa ajili ya kujenga barabara halafu nyie mnataka kumtoza fedha”
Waziri Magufuli aliongeza kuwa kuna watu wa mikoa mingine hawajawai hata kuona rangi ya lami na wangetamani kuwapa hao wachina mawe ili wawajengee barabara, hivyo Halmashauri itatakiwa ibadili uamuzi huo haraka.
Pia Waziri Magufuli amemtaka Mkandarasi huyo wa Kichina kutumia mawe hayo katika ujenzi wa barabara na si vinginevyo.
Katika hatua nyingine Waziri Magufuli amewaasa Wakazi wa Butiama kuilinda Amani iliyopo nchini.
“Baadhi ya nchi nyingine zinajuta kutokana na machafuko yaliyopo mfano Burundi, Misri, Iraq na Libya” Alisema Waziri Magufuli.
WAZIRI WA UJENZI DKT. JOHN MAGUFULI AKISHUKA KUANZA UKAGUZI WA DARAJA LA KYARANO LENYE UREFU WA MITA 53.5 NA UPANA WA MITA 10 KWENYE BARABARA YA MAKUTANO-NYAMUSWA-IKOMA SEHEMU YA MAKUTANO NATTA KM 50.
WAZIRI WA UJENZI DKT. JOHN MAGUFULI WAPILI KUTOKA KUSHOTO AKIPITA KWENYE MOJA YA NGUZO ZA DARALA LA KYARANO KATIKA WILAYA YA BUTIAMA MKOANI MARA.
WAZIRI WA UJENZI DKT. JOHN MAGUFULI AKIENDELEA NA UKAGUZI WA BARABARA YA MAKUTANO-NYAMUSWA-IKOMA SEHEMU YA MAKUTANO NATTA KM 50.
WAZIRI WA UJENZI DKT. JOHN MAGUFULI AKIKAGUA UJENZI WA MAKARAVATI YA DUARA (PIPE CULVERTS) KATIKA ENEO LA MKANDARASI.
WAZIRI WA UJENZI DKT. JOHN MAGUFULI AKISALIMIANA NA MBUNGE WA BUTIAMA NIMROD MKONO BAADA YA KUKAGUA KAZI ZA UFYATUAJI WA MAKARAVATI YA DUARA (PIPE CULVERTS) KATIKA ENEO LA MKANDARASI.
WAZIRI WA UJENZI DKT. JOHN MAGUFULI AKITETA JAMBO NA MBUNGE WA BUTIAMA NIMROD MKONO KABLA YA KUHUTUBIA MAMIA YA WAKAZI WA BUTIAMA KATIKA ENEO LA MAKUTANO KUHUSU UJENZI WA BARABARA YA MAKUTANO NATTA YENYE UREFU WA KILOMITA 50.
WAZIRI WA UJENZI DKT. JOHN MAGUFULI AKIHUTUBIA MAMIA YA WAKAZI WA MAKUTANO KATIKA WILAYA YA BUTIAMA MKOANI MARA.
MAKARAVAT !! Kwa kiswahili yaiantwa MAKALBI ......
ReplyDelete