Kati ya Juni 25 na Julai 6, jiji la Washington DC lilikuwa mwenyeji wa maonyesho ya kila mwaka ya yanayohusu maisha a watu na jamii mbalimbali.
Mwaka huu, nchi ya Kenya ilishirikishwa, wakionyesha utamaduni wao na changamoto za kuzidumisha katika zama hizi za sayansi na teknolojia.
Kwanza Production ilipata fursa ya kutembelea maonyesho hayo na kuzungumza na baadhi ya washiriki wa maonyesho hayo ambapo walieleza mengi ya kufurahisha.
KARIBU UUNGANE NASI

Zaidi ya washiriki 100 kutoka nchini Kenya waLIkuja hapa jijini kuonyesha mambo mbalimbali kama kutengeneza vyungu kwa ufinyanzi, uchongaji vinyago, mapambo ya shanga, useremala, nakshi za majengo, ujenzi wa majahazi, mapishi , muziki na mengine yanayotunza utamaduni wa nchi hiyo
Maelezo ya ujenzi na sehemu za JAHAZI (DHOW) toka kwa Ali Skanda aliyetoka Lamu Kenya
Na mtangazaji mkongwe abdushakur Aboud mbele ya Jahazi lililoletwa kwenye makumbusho ya hapa Washington DC kutoka Lamu nchini Kenya
Mtaalamu wa mapambo yatokanayo na shanga na usimamizi wa filamu nchini Kenya Emmah Irungu
Mwandishi wa habari kutoka Kenya BMJ Mureithi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 14, 2014

    Wenzetu watani wajadi Kenya wametufunga goli la kichwa,watanzania mlio nje vipi? nyinyi amuwezi kufanya ? maana tusiwe kwe siasa tu

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 14, 2014

    wakenya Big Up,sisi watanzania tupo katika siasa na bongo flaver ndio utamaduni wetu

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 14, 2014

    watanzania wangeambiwa waandae hili wangeandaa kongamano la vyama vya kisiasa,na waziri angekuja na timu yake na ndio angewautubia watu hao hao aliofutana nao

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...