Matokeo ya mtihani wa kidato cha 6 yaliyofanyika tarehe Mei 5 – 21, yametoka.
Jumla ya watahiniwa 38,905 sawa na asilimia 95.98 ya watahiniwa
waliofanya mtihani kidato cha 6 wamefaulu. Wasichana waliofaulu ni
12,080 na wavulana waliofaulu ni 26,825.
Watahiniwa waliopata division IV ni 4,420 sawa na asilimia 12.54
Watahiniwa waliopata zero (0) ni 612 sawa na asilimia 1.74.
SHULE 10 ZILIZOONGOZA
1. Igowole
2. Feza Boys
3. Kisimiri
4. Iwawa
5. Kibaha
6. Marian Girls
7. Nangwa
8. Uwata
9. Kibondo
10. Kawawa
SHULE 10 ZA MWISHO
1. Ben Bella
2. Fidel Castro
3. Tambaza
4. MuhezaHigh School
5. Mazizini
6. Mtwara Technical
7. Iyunga technical
8. Al- falaah Muslim
9. Kaliua
10. Osward Mang'ombe
Kuona matokeo pitia hapa: http://www.necta.go.tz/matokeo2014/ACSEE.htm
MATOKEO
KIDATO CHA 6: 95.98% wafaulu kidato cha 6 kutoka 87.9% mwaka jana.
Tambaza ndani ya shule 10 za mwisho, K/Katibu Mtendaji Necta C. Msonde
atangaza leo.
He!! Mambo yenda yakibadilika. Siku hizi Tambaza A-level ni ya mwisho?? Siamini!
ReplyDeleteShule niliyosoma Tambaza ilikuwa inakuwa ya kwanza mpaka tatu, miaka ya 80`s jamani kwa sasa wanafeli mpakasio rahisi kuamini! Mdau hapo juu tupo wote kutoamini!
ReplyDeleteHongera sana na pongezi za dhati kwa walimu, wanafunzi na uongozi mzima wa shule ya sekondari ya Kibondo. Nakumbuka mwanzo ulikuwa mgumu kitaaluma once ilipoanzishwa 'A-level' shuleni hapo, in 1994. Lakini kwa kadri miaka ilivyokuwa ikisonga mbele, kulionekana kuwepo kwa matumaini na maendeleo kitaaluma, hadi leo hii kuwa katika kumi bora ni jambo la fakhari na kujivunia sana. Congratulations and keep it up!
ReplyDeleteNini kimezikuta shule za serikali mpaka zinakua za mwisho.Siamini shule kama Tambaza na Iyunga kuwa za mwisho.
ReplyDeleteWalioshinda hongera waliojikuta hawakufaulu mjipange kusuma gurudumu la maisha mbele..
ReplyDeleteTAMBAZA KWELI SIAMINI
ReplyDeleteDu!! Tambaza!! PCM, PCB ndiko tulikokuwa tunategemea. Du!! I cann't speak anything.
ReplyDelete