Padz Hotel ni kiota kipya kilichoota maeneo ya Forest kwenye Barabara Kuu ya Tanzania-Zambia, jirani na Chuo cha Mzumbe Univeristy, dakika kadhaa toka Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Songwe na katikati ya Jiji la Mbeya.
Alama yake kuu ukitokea Songwe ni bendera za Tanzania na Marekani kwa nje na mjengo wa kioo tupu. Pazuri, huduma bomba msosi ndio usiseme. Na bei ni ya kiwandani...Kuwasiliana nao piga +255252500635 ama +255759851439 na +255652319139 ama email info@padtzhotel,com na pia nenda www.padzhotel.com
Hapo ndo tunaposema ni muhimu sana kusoma Kiswahili shuleni, watu wangeelewa ushauri huu Kiswahili kisinge pinda kama kilivyo pinda kwenye bango hilo.
ReplyDeleteHATUSEMI;"jengo hili la padz hotel Imefunguliwa na mkuu wa mkoa wa Mbeya"hapana.
BADALA YAKE TUNASEMA; "Jengo hili la padz hotel Limefunguliwa na mkuu wa mkoa wa Mbeya"
Kwahiyo katika Kiswahili KITENZI Kufunguliwa kinatakiwa kiangalie kielezi "JENGO HILI" na sio kuangalia NOMINO "hOTEL" hapana.