Na Abdulaziz Video,Lindi.

Viongozi wa Dini wilayani Kilwa mkoani Lindi wametakiwa kuhubiri Amani,umoja na mshikamano wanapokuwapo kwenye ibada zao ili kuliombea Taifa lisiingie kwenye vurugu zinazoweza kusababisha uvunjivu wa amani ya nchi Hususan katika mchakato wa katiba mpya

Akihutubia waislam walioshiriki katika shindano la kila mwaka la Usomaji wa Quran,Mkuu wa wilaya ya kilwa,Abdallah Ulega ameeleza kuwa viongozi wa dini wana nafasi kubwa katika Kuelimisha na kukemea waumini wao kufanya mambo ambayo yanaweza kusababisha kuleta madhara ya kuwagawa watanzania.

Aidha alibainisha kuwa nchi yetu kwa sasa iko katika kipindi cha mpito cha kutafuta katiba ambapo alitumia nafasi hiyo kutoa wito kwa waislam kukemea tabia za Rushwa,wizi,zinaa,Uharibifu wa Mazingira na inawezekana ikiwa Quran itasomwa na kuhifadhiwa kuzingatiwa Ipasavyo "Hakika nyie ni mashuhuda Mwezi huu wa Ramadhan hali ni ya Utulivu sana katika mji wetu hakuna Disco,Rusha Roho pamoja na mikusanyiko katika mabar Tena Hata kimavazi watu wanavaa mavazi ya Heshima hali imekuwa ya Amani sana Naomba waislamu wenzagu msiache Tumche Mola wetu"Alimalizia Ulega.

Kwa upande wake kaimu Shekhe mkuu wa wilaya za Kilwa,Sheikh Muhidin Matuta alisema kuwa ni wajibu wa waislamu kujenga upendo baina yao na pamoja na kufundisha maadili kwa watoto ili wawe viongozi bora wa baadaye.

Aidha Sheikh Muhidin alieleza kuwa shindano hilo linaloratibiwa na kamati ya kusimamia Mashindano ya Quran Kilwa(QUROU)licha ya usimamizi huo tayari inamiliki Ardhi ambayo imekusudiwa kujengwa kwa shule itakayowalea na kuwasomesha Mahafidh wa Quran na viozi jana wengine waweze kuwa miongoni mwa Jamii na Viongozi bora wa Taifa.

"Waislamu wenzangu tupo katika mfungo wa Ramadhan,Mwezi ambao utukufu wake kila mmoja anaujua na jitahada zinafanywa na masheikh na waalimu wa Dini kukumbusha na kuelimisha Faida zinazopatikana katika Mwezi huu hivyo usiaharibu wema wote kwa kufurahia sikukuu ya IDD"Alimalizia kaimu Sheikh wa Wilaya ya Kilwa

Katika shindano hilo Khadija Kaudunde aliibuka na ushindi katika usomaji wa Juzuu 1,Mariam Suleiyman alishindika usomaji wa juzuu 3,Shaweji Mwichande Juzuu 5,Amir Hassan Mkwachu Juzuu 10 huku Abdallah Yusuf Kombo akifanikiwa katika usomaji wa Juzuu 30 Zawadi mbalimbali zilitolewa kwa washindi ikiwemo magodoro,Cherehani,Radio,Baiskeli kwa washindi na walimu wao pamoja na Pesa Taslimu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...