Na Abdulaziz Video,Lindi.
Viongozi wa Dini wilayani Kilwa mkoani Lindi wametakiwa kuhubiri
Amani,umoja na mshikamano wanapokuwapo kwenye ibada zao ili kuliombea
Taifa lisiingie kwenye vurugu zinazoweza kusababisha uvunjivu wa amani
ya nchi Hususan katika mchakato wa katiba mpya
Akihutubia waislam walioshiriki katika shindano la kila mwaka la
Usomaji wa Quran,Mkuu wa wilaya ya kilwa,Abdallah Ulega ameeleza kuwa
viongozi wa dini wana nafasi kubwa katika Kuelimisha na kukemea
waumini wao kufanya mambo ambayo yanaweza kusababisha kuleta madhara
ya kuwagawa watanzania.
Aidha alibainisha kuwa nchi yetu kwa sasa iko katika kipindi cha
mpito cha kutafuta katiba ambapo alitumia nafasi hiyo kutoa wito kwa
waislam kukemea tabia za Rushwa,wizi,zinaa,Uharibifu wa Mazingira na
inawezekana ikiwa Quran itasomwa na kuhifadhiwa kuzingatiwa Ipasavyo
"Hakika nyie ni mashuhuda Mwezi huu wa Ramadhan hali ni ya Utulivu
sana katika mji wetu hakuna Disco,Rusha Roho pamoja na mikusanyiko
katika mabar Tena Hata kimavazi watu wanavaa mavazi ya Heshima hali
imekuwa ya Amani sana Naomba waislamu wenzagu msiache Tumche Mola
wetu"Alimalizia Ulega.
Kwa upande wake kaimu Shekhe mkuu wa wilaya za Kilwa,Sheikh Muhidin
Matuta alisema kuwa ni wajibu wa waislamu kujenga upendo baina yao na
pamoja na kufundisha maadili kwa watoto ili wawe viongozi bora wa
baadaye.
Aidha Sheikh Muhidin alieleza kuwa shindano hilo linaloratibiwa na
kamati ya kusimamia Mashindano ya Quran Kilwa(QUROU)licha ya usimamizi
huo tayari inamiliki Ardhi ambayo imekusudiwa kujengwa kwa shule
itakayowalea na kuwasomesha Mahafidh wa Quran na viozi jana wengine
waweze kuwa miongoni mwa Jamii na Viongozi bora wa Taifa.
"Waislamu wenzangu tupo katika mfungo wa Ramadhan,Mwezi ambao utukufu
wake kila mmoja anaujua na jitahada zinafanywa na masheikh na waalimu
wa Dini kukumbusha na kuelimisha Faida zinazopatikana katika Mwezi huu
hivyo usiaharibu wema wote kwa kufurahia sikukuu ya IDD"Alimalizia
kaimu Sheikh wa Wilaya ya Kilwa
Katika shindano hilo Khadija Kaudunde aliibuka na ushindi katika
usomaji wa Juzuu 1,Mariam Suleiyman alishindika usomaji wa juzuu
3,Shaweji Mwichande Juzuu 5,Amir Hassan Mkwachu Juzuu 10 huku Abdallah
Yusuf Kombo akifanikiwa katika usomaji wa Juzuu 30
Zawadi mbalimbali zilitolewa kwa washindi ikiwemo
magodoro,Cherehani,Radio,Baiskeli kwa washindi na walimu wao pamoja na
Pesa Taslimu
Allah awalipe
ReplyDelete