Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu (kulia) akizungumza na
Balozi wa Heshima wa Utalii wa Tanzania nchini Marekani Bw. Ahmed Issa
juu ya mikakati mbalimbali ya kuvutia watalii wa kimarekani kutembelea
Tanzania jana Beverly, Los Angeles.
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu (kati) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Heshima wa Utalii wa Tanzania nchini Marekani Bw. Ahmed Issa (kushoto) na Bw. Abdul Majid baada ya kupokea taarifa ya mikakati wanayoitumia kutangaza vivutio vya utalii wa Tanzania kwa wamarekani jana Beverly, Los Angeles.
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu (kulia) akiagana na Balozi
wa Tanzania wa Heshima wa Utalii nchini Marekani Bw. Ahmed Issa mara
baada ya kumaliza mazungumzo juu ya masuala kadhaa ya kuvutia Watalii
wa Marekani nchini Tanzania jana Beverly, Los Angeles.
Mikakati inayotumiwa na Balozi wa Heshima wa Utalii wa Tanzania Bw.
Ahmed Issa kutangaza utalii ni pamoja na matumizi ya magari yenye picha
za vivutio vya utalii wa Tanzania katika majiji mbalimbali katika California -
Marekani kama inavyoonekana katika picha.
Kunaitwa Beverly Hills.
ReplyDeleteLazaro rafiki yangu bado mavazi yanakupa wakati mgumu.
ReplyDelete