Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu (kulia) akizungumza na Balozi wa Heshima wa Utalii wa Tanzania nchini Marekani Bw. Ahmed Issa juu ya mikakati mbalimbali ya kuvutia watalii wa kimarekani kutembelea Tanzania jana Beverly, Los Angeles.
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu (kati) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Heshima wa Utalii wa Tanzania nchini Marekani Bw. Ahmed Issa (kushoto) na Bw. Abdul Majid baada ya kupokea taarifa ya mikakati wanayoitumia kutangaza vivutio vya utalii wa Tanzania kwa wamarekani jana Beverly, Los Angeles.
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu (kulia) akiagana na Balozi wa Tanzania wa Heshima wa Utalii nchini Marekani Bw. Ahmed Issa mara baada ya kumaliza mazungumzo juu ya masuala kadhaa ya kuvutia Watalii wa Marekani nchini Tanzania jana Beverly, Los Angeles.
Mikakati inayotumiwa na Balozi wa Heshima wa Utalii wa Tanzania Bw. Ahmed Issa kutangaza utalii ni pamoja na matumizi ya magari yenye picha za vivutio vya utalii wa Tanzania katika majiji mbalimbali katika California - Marekani kama inavyoonekana katika picha.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 19, 2014

    Kunaitwa Beverly Hills.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 19, 2014

    Lazaro rafiki yangu bado mavazi yanakupa wakati mgumu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...