Mtaalamu wa kujadili mikataba kutoka World Trade
Organization (WTO), Prof. Dickson Yeboah akitoa mada jijini Dar es Salaam
wakati wa mkutano wa Kimataifa wa kuwajengea uwezo maofisa wa serikali kutoka
nchi 15 za Afrika Mashariki, Afrika ya Kati na Afrika Kusini kuhusu uandikaji
wa mikataba inayohusu Uwekezaji na Biashara. Mkutano huo umeandaliwa na Chuo
Kikuu cha Bagamoyo.
Na Happiness Katabazi
CHUO Kikuu cha Bagamoyo (UB), kimesema kitaendelea kuandaa mafunzo ya jinsi ya Kutengeneza mikataba na wawekezaji kwa maofisa wa serikali za nchi zinazoendelea ili serikali hizo ziondokane na tatizo la kuandika mikataba ya uwekezaji ambayo haiziletei faida nchi zao.
Akizungumza na Katika Mafunzo yanayoshirikisha wataaluma wa masuala ya Biashara toka nchi 15 yanayofanyika Katika Hotel ya Habour View Dar Es Salaam ambapo Mafunzo hayo yameandaliwa na Chuo Kikuu Cha Bagamoyo na kufadhiliwa na Chuo Kikuu Cha Nordic Africa Institute of the University of Uppsala Cha nchini Sweden, Mkuu wa Shule ya Biashara na Utawala (UB), Dk.Lenny Kasoga Alisema Mafunzo ya wiki mbili yameusisha maofisa wa juu wa serikali mbalimbali ambao ni wataalamu wa fani ya Biashara toka nchi 15.
Dk.Kasoga alisema Leo Dunia ipo Karne ya 21 lakini bado nchi zinazoendelea ambazo zimegundulika Kuwa na utajiri mkubwa zimejikuta zikiingia mikataba mibovu na wawekezaji KWA Sababu tu nchi hizo Hazina wataaluma serikalini ambao wamebobea Katika kufanya mijadala ya Kibiashara na wawekezaji na jinsi ya kuandika mikataba hiyo.
"Kwa kukuona tatizo Hilo sisi UB, tumeandaa Mafunzo haya ambayo yamewapa mwanga maofisa Hao waandamizi toka serikali za nchi 15 ambapo Mafunzo tuliyowapatia watayapeleka Katika serikali zao na vyuo vyao ili waweza kuandaa mitaala Katika vyuo vikuu vyao NGazi ya Shahada ya Pili ili watu wasome' Alisema Dk.Kasoga.
ALizitaja nchi zinazoshiriki Mafunzo ambayo ni ya kwanza kufanyika nchini ambayo yanatarajiwa Kufungwa Ijumaa ya wiki hii na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk.Shukuru Kawambwa Ni Mwenyeji Tanzania na Zanzibar, Madagascar,Mozambique, Rwanda,Malawi,Zambia, Burundi, Uganda, Ethiopia ,Kenya, Kongo, Malawi na Lesotho.
Kwa upande wake Profesa Francis Matambalya toka Chuo Kikuu Cha NAI, Uppsalla nchini Sweed, alisema chuo chao wameamua kufadhili UB iendeshe Mafunzo hayo kwasababu wanaamini UB ninauwezo wa kuendesha Mafunzo na kwamba Tanzania pia ambayo Katika Mafunzo hayo wamewasilisha na maofisa Biashara toka Wizara ya Viwanda na Biashara nayo inamkabili na Changamoto hiyo.
Hivi ni kwa nini baadhi ya waandishe wetu huwa hampendi kutumia maneno au misamiati muafaka inayoendana sambamba na tukio au mazingira husika? Ni uhaba wa misamiati ya kiswahili au kutofaham maana zake. Nimesema hivyo kwa sababu ya hilo neno lililotumika hapo 'Kufunda' nadhani halikustahili hapo, japokuwa imeeleweka, lakini kwa uandishi na utumiaji wa maneno/misamiati ya kiswahili ulio fasaha, basi hapo si pahala pake, angalau lingetumika neno mathalan...Chuo kikuu cha Bagamoyo 'chawanowa' maofisa... lakini sio chawafunda... neno hilo lina mazingira yake na pahala pake maalum pa kulitumia na likakubalika zaidi kuliko lilivyotumiwa hapo.
ReplyDeleteSamahani wahusika mana naamini baadhi yetu huwa wanakereka sana wanapokosolewa au kurekebishwa katika kazi zao.
Kweli mdau wa kwanza hapo juu yaani Globu ya Jamii imekuwa kama ''Magazeti- Pendwa''.
ReplyDeleteHabari inayozungumzia shughuli ya maana kama hii inabidi iendane sawia na lugha/uandishi makini.
Mdau
Christos Papachristou
Diaspora.
Ndugu HK
ReplyDeleteNashukuru kwa niaba ya UB na mwandishi wetu kwa ukosoaji wako wenye nia njema.
Tutazingatia ushauri wako mzuri kila tutakapoandaa makala mengine juu ya mafunzo yetu ya kuwanoa maafisa na watu wengine.
EGM