Mwanamitondo afanyae kazi zake za mitindo nchini Marekani Flaviana Matata, yuko nchini kwa ajili ya kufanya kazi za kijamii kupitia taasisi yake ya Flaviana Matata Foundation. katika mradi wa Back to school project /FMFstationarykit ambao unafadhiliwa na mfuko wa penseni PSPF,
Baada ya mwezi January Flaviana kugawa vifaa shule za msingi za jijini awamu hii ameenda Mtwara na kufanikiwa kugawa shule za Msingi Mtua na Chemchem ziliyopo Nachingwea pamoja nashule za msingi Litingi na Mnengulo ziliyopo Lindi.
bado wanaendelea kugawa vifaa hivyo kwa shule za msingi mikoa mingine "hadi sasa tumeshagawa vifaa kwa watoto 700 na bado kuna kits 800 vitasambazwa Tunduma ,Tunduru na Monduli"
Flaviana alitoa shukran kwa PSPF kwa kudhamini huu mradi na akasisitiza makampuni na mashirika kujaribu kuwezesha elimu kama hali halisi inavyoonekana kwenye picha hadi leo kuna wanafunzi wanasoma chini na mti, na walio madarasani,madarasa ni mabovu na hayana madawati.







Walimu na bodi za shule wakisaidiwa na halmashauri zinazohusika wangekuwa wana mipango rya kuboresha miundo mbinu ya shule kwa kuhamasisha wazazi na kufanya michango inayohusisha wengine kila mwaka kwa mfano wakati wa mahafali madarasa yangekuwa yamejengwa, madawati yangekuwepo, ofisi za walimu bora kuliko hizo za udongo, na matundu ya vyoo yanayosikika kwenye risala kila wakati tusingekuwa tunayazungumzia mambo kama haya wakati huu miaka hamsini baada ya uhuru. Sehemu nyingine haya yanafanyika kwanini wengine hawana mikakati ya kuboresha mazingira ya shule zao.
ReplyDelete