Kaka michuzi naomba unichapishie makala yangu kwenye blog yako. Kama
tunavyofahamu kwa wakati huu Tanzania ipo katika mgogoro wa ziwa nyasa kati yetu na
Malawi wenzetu wameenda mbali zaidi kwa kutumia mtandao wa Google Map.
Google
Map ni mtandao mkubwa ambo unaonyesha Ramani ya dunia nzima kwa kutumia picha
ya satellite na watu wengi hususani watalii hutumia mtandao huu kabla ya kwenda
mahali husika . Lakini mtandao huu huitaji watu kujaza taarifa zaidi kama kuonyesha
mipaka ya mikoa nchi na maeneo mbalimbali. Kama ilivyo kwa nchi nyingine duniani
ambao huchukulia jambo ili kwa manani na kulipa kipaumbele lakini hiyo imekua
tofauti kwa Tanzania.
Ukiangalia kwenye mtandao huu kwa sasa utaona Ziwa Nyasa linaitwa Ziwa Malawi na
pia mipaka inaonyesha mpaka wa nchi ya Malawi upo hadi pembezoni mwa ziwa nyasa
kama madai yao yalivyo yaani eneo la Tanzania.
Hii inasikitisha sana kwa sababu serekali imeajiri wataalumu wengi wenye uwezo wa
kuzijaza taarifa hizo kwenye mtandao huo na kwenye mitandao mingine duniani kwa ajili
ya kulinda tunu za taifa letu lakini hali imekua ni tofauti.
Hii si mara ya kwanza Mali ya
Tanzania kufanyiwa hivyo kwa mfano Mlima Kilimanjaro kuna wakati ulionyeshwa au
kuta tangazwa kama upo Kenya na pia lugha ya Kiswahili kwa sasa inaandikwa kwenye
vitu mbali mbali hususani kwenye programu mbalimbali za computer ambazo zina
uchaguzi wa lugha mbalimbali hususani kampuni kubwa ya Microsoft. Hii inaonyesha ni
jinsi gani taifa letu lilivyolala na kupigana vita vya maneno tu badala ya kupigana kwa
vitendo.
Swala hili ni kubwa ambalo serekali inapaswa kulichukuli hatua kwa sababu kwa sisi
tuliopo sasa tunajua kwamba ni upotoshaji lakini kwa vizazi vitakavyokuja miaka mingi
ijayo vitaichukulia kama hiyo ni taarifa sahii na hivyo itakuja kuligharimu hata taifa letu
la Tanzania
Kwa kupitia makala hii namwomba Rais wa jamuhuri ya Muungano Mh Kikwete
kulichukulia swala hili kwa uzito unaohitajika na hata ikiwezekana kufuatilia kwenye
kampuni ya Google ili taarifa hizi zibadilishwe maana ni upotoshaji mkubwa.
Pia
napenda kuwakumbusha wataalamu wenzangu ambao mmeajiriwa kati wizara
mbalimbali husika muwe pia makini na mitandao mbalimbali duniani kujaza taarifa
muhimu za nchi yetu kwenye mifumo hiyo, nawaombeni tuwe wabunifu.
Ni mimi Mtanzania
Emmanuel Millinga
Millinga_emmanuel@yahoo.com
0715 817788
Viongozi wetu kuchekecheka kila wakati wafanyakazi wao soga na kula vitumbua ofisini kazi IPO kwelikweli
ReplyDeleteHizo taarifa zinajazwa vp? Si nasisi tujaze kama tunavyotaka ili tuone watafanya nini.
ReplyDeleteNakushauri na wewe ujaze tuu kama unaweza. Ukishindwa niambie mimi jinsi ya kujaza, then nitajaza.
Hili swala hakuna kusubiria serikali au watu wahusika.
Sisi ndio wahusika wakuu.
Hongera kwa kuliona hili
Ukiangalia vizuri utaona kuwa ktk mpaka huo alama zimeonyeshwa kwa dots maana yake kuwa kuna mashaka ktk mpaka husika. Pia kitu hicho kinaonekana ktk mpaka wa DRC na Congo Brazaville kwani kila mmoja mto Kongo wote upo upande wake. Kinachotakiwa kufanyika ni serikali kulalamika rasmi Google kuwa mpaka uwekwe katikati ukiwa na hizo dots kwani zinachanganya baadhi ya watu. Sijui nhusika ni wizara ipi bali nchi nyingine zimefanya hivyo pindi zinapoona kuwa kuna ubabaishaji ktk ramani.
ReplyDeleteNyati
Siyo vitumbua tu ukiingia ofisi za Tanzania nyeti zenye komputa unaweza kulia. ni kula vitumbua na chipsi kuku tu nyuma ya computer na kazi ya computer ni facebook na mitandao ya kijamii hadi kilio. hilo swala la google map hata mi nilishaliona siku sikujua utaratibu unaotumika kuingiza maps kwenye google.watanzania tubadirikeni tuwe serious na issue za kitaifa
ReplyDeletemdau UK
Heri mimi sijasema.....manenge...hahahaha ukisema utaambiwa mchonganishi au una lugha zenye kuudhi......
ReplyDeleteNakubali kuna haja ya kuchukua hatua. Lakini nasi tusikiharibu kiswahili chetu. Swala ni mnyama. Jambo linaitwa Suala. Tujirekebishe na tukienzi Kiswahili chetu.
ReplyDeleteNadhani nadhani ndugu aliyecomment hapo pia hana uelewa wa kutosha. Swala la mpaka wa Tanzania Malawi haliwezi kuwa judged kwa la "ziwa malawi" jina hilo lina sababu nyingi za kihistoria, rejea "scramble ana partition of Africa" ktk historia. Alafu si kweli kwamba watu hawajui matumizi ya google map bali mipaka mingi inayohusisha water bodies zinaomgozwa na sheria za kimataifa hivyo ni sawa kwa serikali kutumia wataalamu na lazima
ReplyDeleteUjiulize kwanini swala hili la mipaka limekuja wakati huu, zaidi ya miaka 50 baada ya uhuru?
Ndugu zanguni kitaalamu mpaka unapochorwa na dot dot maana yake huo mpaka haujathibitishwa. Kwa sababu kuna hatua tatu ya kwanza ni kuchora kama walivyofanya wakoloni, pili ni rectification na tatu ni reaffirmation hatua hizo ambazo hawakuzifanya. Ndio maana katika hoja ambazo Tanzania inawaambia. Malawi ni hatua hizo mbili zifanyike. Sio kweli viongozi wenu wanacheka cheka. Kwani google ndio mamlaka husika ya kutuvhorea mpaka wetu? Viongozi wa Tanzania wanafanya kazi sana sana juu ya suala hilo. Ninawashauri acheni lawama na kejeli! Wahusika wanavhapa kazi bwana!
ReplyDeleteNashukurumowa ushauri wako ndugu mwenye makala hapo juu.Lakini suala na Tz na Malawi ni zaidi ya google map, ni suala la kihistoria na kisheria hivyo ni haki saana tena sana serikali kutumia wataalamu hata google map si jambo geni na si kwamba serikali haijui na zaidi migogoro ya mipaka si kwa Tz na Malawi tu ni sehemu nyingi za dunia na hazikuamuliwa kwa google map.
ReplyDeleteMdau
Mdau mwenye makala hapo juu lazima ajua suala la mipaka la Tz na Malawi ni suala zaidi ya google map, ni suala la kihistoria na kisheria na ni haki kwa serikali kutumia wataalamu hao na si kweli kwamba hawajui technology ya google map.
ReplyDeleteMdau
Nashukuru kwa mawazo ya kujenga ya mdau hapo juu.
ReplyDeleteNashukuru kwa mawazo ya kujenga ya mdau hapo juu.
ReplyDeletehongera kaka kwa kuliona hili...kama unaweza hebu saidia nchi yako jaza hizo info.. maana hapo baadaye hili litakuwa janga kubwa .. ni kama kiswahili huku uk wakenya wanajitangaza wao ndio wamiliki wakuu tz tumeiga na wazungu wanajua hivo tz hatujui kiswahili.. limekuwa janga huwa inaniuma twapoteza ving wa tz..
ReplyDeleteNi kweli wadau hili la watumishi wa serikali/ na wasio wa serikali kuegemea kat mitandao ya kijamii ni ukweli 100%.
ReplyDeleteHivi haiwezekani kuwa na mfumo wa kuzifunga(Ku block),
Tanzania tuna safari ndefu kufika kuleee wenzetu walipo.
Wacha wamalawi waendelee kuchorachora kwenye Google,hiyo haituondolei usingizi.Tunasubiri watakapo weka bendera au kuwafukuza, kuwanyanyasa raia wetu katika maeeneo yetu hapo ndipo litakuwa jambo.
ReplyDeletewadau mnaoulizia namna ya kuedit mipaka au features nyingine kwenye google maps, mnatakiwa kuji register hasa kwa kutumia gmail then unafungua Google Map Maker. Huko unaweza kuweka barabara, maeneo muhimu kama kanisa shule nk hata hilo la mipaka ingawa ni la kisheria zaidi na pia linahusisha wataalam zaidi ila nadhani linaweza kuwekwa then wenyewe wata confirm
ReplyDelete