Kaka michuzi naomba unichapishie makala yangu kwenye blog yako. Kama tunavyofahamu kwa wakati huu Tanzania ipo katika mgogoro wa ziwa nyasa kati yetu na Malawi wenzetu wameenda mbali zaidi kwa kutumia mtandao wa Google Map.

Google Map ni mtandao mkubwa ambo unaonyesha Ramani ya dunia nzima kwa kutumia picha ya satellite na watu wengi hususani watalii hutumia mtandao huu kabla ya kwenda mahali husika . Lakini mtandao huu huitaji watu kujaza taarifa zaidi kama kuonyesha mipaka ya mikoa nchi na maeneo mbalimbali. Kama ilivyo kwa nchi nyingine duniani ambao huchukulia jambo ili kwa manani na kulipa kipaumbele lakini hiyo imekua tofauti kwa Tanzania.

Ukiangalia kwenye mtandao huu kwa sasa utaona Ziwa Nyasa linaitwa Ziwa Malawi na pia mipaka inaonyesha mpaka wa nchi ya Malawi upo hadi pembezoni mwa ziwa nyasa kama madai yao yalivyo yaani eneo la Tanzania.

Hii inasikitisha sana kwa sababu serekali imeajiri wataalumu wengi wenye uwezo wa kuzijaza taarifa hizo kwenye mtandao huo na kwenye mitandao mingine duniani kwa ajili ya kulinda tunu za taifa letu lakini hali imekua ni tofauti.

Hii si mara ya kwanza Mali ya Tanzania kufanyiwa hivyo kwa mfano Mlima Kilimanjaro kuna wakati ulionyeshwa au kuta tangazwa kama upo Kenya na pia lugha ya Kiswahili kwa sasa inaandikwa kwenye vitu mbali mbali hususani kwenye programu mbalimbali za computer ambazo zina uchaguzi wa lugha mbalimbali hususani kampuni kubwa ya Microsoft. Hii inaonyesha ni jinsi gani taifa letu lilivyolala na kupigana vita vya maneno tu badala ya kupigana kwa vitendo.

Swala hili ni kubwa ambalo serekali inapaswa kulichukuli hatua kwa sababu kwa sisi tuliopo sasa tunajua kwamba ni upotoshaji lakini kwa vizazi vitakavyokuja miaka mingi ijayo vitaichukulia kama hiyo ni taarifa sahii na hivyo itakuja kuligharimu hata taifa letu la Tanzania

Kwa kupitia makala hii namwomba Rais wa jamuhuri ya Muungano Mh Kikwete kulichukulia swala hili kwa uzito unaohitajika na hata ikiwezekana kufuatilia kwenye kampuni ya Google ili taarifa hizi zibadilishwe maana ni upotoshaji mkubwa.

Pia napenda kuwakumbusha wataalamu wenzangu ambao mmeajiriwa kati wizara mbalimbali husika muwe pia makini na mitandao mbalimbali duniani kujaza taarifa muhimu za nchi yetu kwenye mifumo hiyo, nawaombeni tuwe wabunifu. Ni mimi Mtanzania Emmanuel Millinga Millinga_emmanuel@yahoo.com 0715 817788

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. Viongozi wetu kuchekecheka kila wakati wafanyakazi wao soga na kula vitumbua ofisini kazi IPO kwelikweli

    ReplyDelete
  2. Hizo taarifa zinajazwa vp? Si nasisi tujaze kama tunavyotaka ili tuone watafanya nini.

    Nakushauri na wewe ujaze tuu kama unaweza. Ukishindwa niambie mimi jinsi ya kujaza, then nitajaza.

    Hili swala hakuna kusubiria serikali au watu wahusika.

    Sisi ndio wahusika wakuu.

    Hongera kwa kuliona hili

    ReplyDelete
  3. Ukiangalia vizuri utaona kuwa ktk mpaka huo alama zimeonyeshwa kwa dots maana yake kuwa kuna mashaka ktk mpaka husika. Pia kitu hicho kinaonekana ktk mpaka wa DRC na Congo Brazaville kwani kila mmoja mto Kongo wote upo upande wake. Kinachotakiwa kufanyika ni serikali kulalamika rasmi Google kuwa mpaka uwekwe katikati ukiwa na hizo dots kwani zinachanganya baadhi ya watu. Sijui nhusika ni wizara ipi bali nchi nyingine zimefanya hivyo pindi zinapoona kuwa kuna ubabaishaji ktk ramani.

    Nyati

    ReplyDelete
  4. Siyo vitumbua tu ukiingia ofisi za Tanzania nyeti zenye komputa unaweza kulia. ni kula vitumbua na chipsi kuku tu nyuma ya computer na kazi ya computer ni facebook na mitandao ya kijamii hadi kilio. hilo swala la google map hata mi nilishaliona siku sikujua utaratibu unaotumika kuingiza maps kwenye google.watanzania tubadirikeni tuwe serious na issue za kitaifa

    mdau UK

    ReplyDelete
  5. Heri mimi sijasema.....manenge...hahahaha ukisema utaambiwa mchonganishi au una lugha zenye kuudhi......

    ReplyDelete
  6. Nakubali kuna haja ya kuchukua hatua. Lakini nasi tusikiharibu kiswahili chetu. Swala ni mnyama. Jambo linaitwa Suala. Tujirekebishe na tukienzi Kiswahili chetu.

    ReplyDelete
  7. Nadhani nadhani ndugu aliyecomment hapo pia hana uelewa wa kutosha. Swala la mpaka wa Tanzania Malawi haliwezi kuwa judged kwa la "ziwa malawi" jina hilo lina sababu nyingi za kihistoria, rejea "scramble ana partition of Africa" ktk historia. Alafu si kweli kwamba watu hawajui matumizi ya google map bali mipaka mingi inayohusisha water bodies zinaomgozwa na sheria za kimataifa hivyo ni sawa kwa serikali kutumia wataalamu na lazima
    Ujiulize kwanini swala hili la mipaka limekuja wakati huu, zaidi ya miaka 50 baada ya uhuru?

    ReplyDelete
  8. Ndugu zanguni kitaalamu mpaka unapochorwa na dot dot maana yake huo mpaka haujathibitishwa. Kwa sababu kuna hatua tatu ya kwanza ni kuchora kama walivyofanya wakoloni, pili ni rectification na tatu ni reaffirmation hatua hizo ambazo hawakuzifanya. Ndio maana katika hoja ambazo Tanzania inawaambia. Malawi ni hatua hizo mbili zifanyike. Sio kweli viongozi wenu wanacheka cheka. Kwani google ndio mamlaka husika ya kutuvhorea mpaka wetu? Viongozi wa Tanzania wanafanya kazi sana sana juu ya suala hilo. Ninawashauri acheni lawama na kejeli! Wahusika wanavhapa kazi bwana!

    ReplyDelete
  9. Nashukurumowa ushauri wako ndugu mwenye makala hapo juu.Lakini suala na Tz na Malawi ni zaidi ya google map, ni suala la kihistoria na kisheria hivyo ni haki saana tena sana serikali kutumia wataalamu hata google map si jambo geni na si kwamba serikali haijui na zaidi migogoro ya mipaka si kwa Tz na Malawi tu ni sehemu nyingi za dunia na hazikuamuliwa kwa google map.
    Mdau

    ReplyDelete
  10. Mdau mwenye makala hapo juu lazima ajua suala la mipaka la Tz na Malawi ni suala zaidi ya google map, ni suala la kihistoria na kisheria na ni haki kwa serikali kutumia wataalamu hao na si kweli kwamba hawajui technology ya google map.
    Mdau

    ReplyDelete
  11. Nashukuru kwa mawazo ya kujenga ya mdau hapo juu.

    ReplyDelete
  12. Nashukuru kwa mawazo ya kujenga ya mdau hapo juu.

    ReplyDelete
  13. hongera kaka kwa kuliona hili...kama unaweza hebu saidia nchi yako jaza hizo info.. maana hapo baadaye hili litakuwa janga kubwa .. ni kama kiswahili huku uk wakenya wanajitangaza wao ndio wamiliki wakuu tz tumeiga na wazungu wanajua hivo tz hatujui kiswahili.. limekuwa janga huwa inaniuma twapoteza ving wa tz..

    ReplyDelete
  14. Ni kweli wadau hili la watumishi wa serikali/ na wasio wa serikali kuegemea kat mitandao ya kijamii ni ukweli 100%.
    Hivi haiwezekani kuwa na mfumo wa kuzifunga(Ku block),

    Tanzania tuna safari ndefu kufika kuleee wenzetu walipo.

    ReplyDelete
  15. Wacha wamalawi waendelee kuchorachora kwenye Google,hiyo haituondolei usingizi.Tunasubiri watakapo weka bendera au kuwafukuza, kuwanyanyasa raia wetu katika maeeneo yetu hapo ndipo litakuwa jambo.

    ReplyDelete
  16. Mdau LubidaAugust 10, 2014

    wadau mnaoulizia namna ya kuedit mipaka au features nyingine kwenye google maps, mnatakiwa kuji register hasa kwa kutumia gmail then unafungua Google Map Maker. Huko unaweza kuweka barabara, maeneo muhimu kama kanisa shule nk hata hilo la mipaka ingawa ni la kisheria zaidi na pia linahusisha wataalam zaidi ila nadhani linaweza kuwekwa then wenyewe wata confirm

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...