Waziri
Mkuu, Mh. Mizengo Pinda kesho, Jumamosi Agosti 23, 2014 anatarajiwa kukagua
ujenzi wa kiwanja wa Ndege wa Mwanza unaopanuliwa miundombinu na majengo ili
kuwezesha ndege kubwa za safari za mizigo zinazolingana na BOEING 747 (CODE D to CODE E) kutua na pia kuhudumia abiria zaidi
ya milioni 2 katika jengo jipya la abiria. Waziri Mkuu atakuwa mkoani hapa
Mwanza kwa ziara ya kiserikali kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo na
kushiriki kama mgeni rasmi katika shughuli za BWM Foundation..
Uwanja
wa ndege wa Mwanza unapanuliwa kwa gharama ya sh,. Bilioni 105. Kati ya fedha
hizo, Serikali ya Tanzania inatoa sh. Bilioni 85 na benki ya BADEA na Shirika
la OFID kwa pamoja (sh. Bilioni 20) zikiwa ni mkopo.
Maeneo
ambayo Waziri Mkuu, Mh. M.K. Pinda anatarajiwa kukagua ni jengo la kuongozea
ndege (control tower), njia ya kurukia na kutua ndege inayorefushwa kwa mita
500 zaidi kutoka mita 3,300 za sasa ili kuwezesha ndege kubwa za mizigo za
Boeing 747 kutua na kuruka katika uwanja huo bila matatizo.
Eneo
lingine litakalotembelewa na Waziri Mkuu ni la mtambo wa lami (asphalt plant) itakayozalisha
lami inayotumika kujenga barabara inayorefushwa ya kuruka na kutua ndege.Mtambo huu unamilikiwa na mkandarasi wa
mradi huu, kampuni ya Beijing Construction Engineering Group ya China.
Mhandisi Mshauri wa mradi huo ni Kampuni ya
United Engineering and Technical Construction (UNETEC) ya Umoja wa Falme za
Kiarabu (UAE) inayofanya kazi ya usanifu na usimamizi wa mradi kwa gharama ya dola za Marekani 3,376,031.00.
Akiwa
uwanjani hapo katika ziara itakayoanza saa 3.00 asubuhi kesho, Jumamosi, Waziri
Mkuu, Pinda anatarajiwa kupata taarifa
ya maendeleo ya mradi huo wa ujenzi kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) wanaojenga miundombinu hiyo ya usafiri wa
anga.
Kazi
ya ujenzi ilianza Julai 2012 na mkataba wa kazi na mkandarasi ulisainiwa Juni
2012. Awali muda wa kumaliza kazi ulipangwa uwe miezi 24 , yaani mwishoni mwa
mwaka huu 2014 lakini kutokana na ufinyu wa bajeti ya serikali sasa kazi
itamalizika Oktoba 2015.. Kazi zinazofanyika mpaka sasa ni urefushaji wa njia
ya kurukia ndege na kutua, upanuzi wa maegesho ya ndege za abiria, ujenzi wa
jengo la abiria na miundombinu yake(barabara ya kuingia na kutoka kwenye
maegesho).
Nyingine
ni ujenzi wa jengo la mizigo, ,maegesho ya ndege za mizigo, jengo la kuongozea ndege,
kituo cha umeme, maegesho ya magari , mifumo ya maji ya mvua na mifumo wa maji safi na taka kwa ajili ya kiwanja
kizima.
Ujenzi
huu utakapokamilika utaufanya uwanja wa ndege wa Mwanza kuwa kitovu cha usafiri
wa anga kwa nchi za maziwa makuu na
kuwezesha ndege za kimataifa (intercontinental flights) kutua.
Pia
utaongeza uwezo wa jengo la abiria
kuhudumia abiria na mizigo kutoka abiria
500,000 kwa mwaka hadi abiria milioni 2 kwa mwaka.
Upanuzi
wa kiwanja cha ndege cha Mwanza ni utekelezaji
wa ahadi ya Rais Jakaya Kikwete kwa wakazi wa Kanda ya Ziwa wakati wa
kampeni za uchaguzi mkuu wa 2010.
TAA inasimamia viwanja 58 yya ndege vya serikali,
inajenga vipya na kuendeleza vilivyopo ambapo hivi sasa inaendelea na ujenzi wa jengo la tatu la abiria kwenye
uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyrere (JNIA), Dar Es Salaam, lenye
uwezo wa kuhudumia abiria milioni 6 kwa mwaka. Jengo hilo la kisasa linajengwa
na mkandarasi, BAM International ya Uholanzi na linatarajiwa kukamilika Oktoba
2015.
Aidha,
TAA imekamilisha miradi kadhaa ukiwemo wa kiwanja cha ndege cha Mpanda, Mafia
na cha Songwe, Mbeya.
IMETOLEWA NA GODFREY JOHN LUTEGO
AFISA
UHUSIANO - OFISI YA SHERIA NA UHUSIANO TAA
(TEL. O713-507777)
Ile terminal building ya Mwanza ilkibadilika itakuwa maendeleo.
ReplyDelete