Mtendaji
Mkuu wa Ofisi ya Rais-Usimamizi wa Utekezaji wa Miradi (PDB) inayosimamia
Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN), Bw. Omari Issa akifafanua jambo wakati wa
mkutano wa awali wa maandalizi ya kujadili vipaumbele vya sekta ya afya vitakavyoingizwa
katika BRN. Mkutano huo wa siku nne umeanza jijini Dar es Salaam leo Jumanne.
Kushoto ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid.
Mkurugenzi
wa SIKIKA, Bw. Irinei Kiria akiwasilisha mada kuhusu sekta ya afya wakati wa
mkutano wa awali wa maandalizi ya kujadili vipaumbele vya sekta ya afya
vitakavyoingizwa katika Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN). Mkutano huo wa
siku nne umeanza jijini Dar es Salaam leo Jumanne. katika ukumbi wa Kunduchi
Beach Hotel and Resort.
Baadhi
ya washiriki wakifuatilia mada wakati wa mkutano wa awali wa maandalizi ya
kujadili vipaumbele vya sekta ya afya vitakavyoingizwa katika Mpango wa Matokeo
Makubwa Sasa (BRN). Mkutano huo wa siku nne umeanza jijini Dar es Salaam leo
Jumanne katika ukumbi wa Kunduchi Beach Hotel and Resort.
Washiriki wakifuatilia mada wakati wa mkutano wa awali wa maandalizi ya kujadili vipaumbele vya sekta ya afya vitakavyoingizwa katika Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN).
Hatua nane za kisayansi zinazotumiwa na Mpango wa BRN katika kuhakikisha wananchi wanapata mafanikio ya haraka katika miradi iliyochaguliwa zilipowakilishwa na Mkurugenzi wa Mipango wa PDB, Bw. Gerase Kamugisha (hayupo pichani) wakati wa maandalizi ya kujadili vipaumbele vya sekta ya afya vitakavyoingizwa katika Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN). Mkutano huo wa siku nne umeanza jijini Dar es Salaam leo Jumanne katika ukumbi wa Kunduchi Beach Hotel and Resort.
Changamoto ya Ebola iliyokumba mataifa mbalmbali Afrika Magharibi nayo ituhamasishe kuwekeza na kuboresha katika miundombinu na huduma za sekta ya Afya
ReplyDelete