Mtendaji Mkuu wa Ofisi ya Rais-Usimamizi wa Utekezaji wa Miradi (PDB) inayosimamia Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN), Bw. Omari Issa akifafanua jambo wakati wa mkutano wa awali wa maandalizi ya kujadili vipaumbele vya sekta ya afya vitakavyoingizwa katika BRN. Mkutano huo wa siku nne umeanza jijini Dar es Salaam leo Jumanne. Kushoto ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid.
 Mkurugenzi wa SIKIKA, Bw. Irinei Kiria akiwasilisha mada kuhusu sekta ya afya wakati wa mkutano wa awali wa maandalizi ya kujadili vipaumbele vya sekta ya afya vitakavyoingizwa katika Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN). Mkutano huo wa siku nne umeanza jijini Dar es Salaam leo Jumanne. katika ukumbi wa Kunduchi Beach Hotel and Resort. 
 Baadhi ya washiriki wakifuatilia mada wakati wa mkutano wa awali wa maandalizi ya kujadili vipaumbele vya sekta ya afya vitakavyoingizwa katika Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN). Mkutano huo wa siku nne umeanza jijini Dar es Salaam leo Jumanne katika ukumbi wa Kunduchi Beach Hotel and Resort.

 Washiriki wakifuatilia mada wakati wa mkutano wa awali wa maandalizi ya kujadili vipaumbele vya sekta ya afya vitakavyoingizwa katika Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN).
 Hatua nane za kisayansi zinazotumiwa na Mpango wa BRN katika kuhakikisha wananchi wanapata mafanikio ya haraka katika miradi iliyochaguliwa zilipowakilishwa na Mkurugenzi wa Mipango wa PDB, Bw. Gerase Kamugisha (hayupo pichani) wakati wa  maandalizi ya kujadili vipaumbele vya sekta ya afya vitakavyoingizwa katika Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN). Mkutano huo wa siku nne umeanza jijini Dar es Salaam leo Jumanne katika ukumbi wa Kunduchi Beach Hotel and Resort.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Changamoto ya Ebola iliyokumba mataifa mbalmbali Afrika Magharibi nayo ituhamasishe kuwekeza na kuboresha katika miundombinu na huduma za sekta ya Afya

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...