Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Gaudensia Simwanza(kushoto) akiwaeleza waandishi wa kuhusu udhibiti wa vyakula vilivyoongezwa virutubisho wakati wa mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari(MAELEZO) leo Jijini Dar es salaam. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari Bi. Zamaradi Kawawa.
Na Frank Mvungi
Serikali imejipanga kufanikisha mpango wa Kitaifa wa urutubishaji vyakula na kusimamia usalama wa vyakula vilivyoongezwa virutubishi kwa lengo la kulinda afya ya walaji.
Hayo yamesemwa na Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini (TFDA) bi Gaudensia Simwanza wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.
Akifafanua Gaudensia amesema TFDA imeandaa kanuni za uongezaji virutubishi kwenye vyakula (Tanzania food, Drugs and Cosmetics (food fortification) Regulations 2012)
Alisema kuwa hatua nyingine ni kuandaa miongozo ya udhibiti wa ubora na usalama wa vyakula vilivyoongezwa virutubishi ili kuwajengea uwezo wasindikaji kuweza kutekeleza matakwa ya kanuni za uongezaji virutubishi kwenye vyakula.
Akifafanua  Gaudensia alisema kuwa  upo mwongozo wa uhakiki wa ubora na usalama katika usindikaji wa mafuta ya kula yaliyoongezwa virutubishi na mwongozo wa uhakiki wa ubora na usalama katika usindikaji wa unga wa mahindi ulioongezwa virutubishi ili kuliunda afya ya mlaji.
Katika hatua nyingine Gaudensia alibainisha kuwa mwongozo wa usimamizi wa Kanuni za uongezaji virutubishi na mwongozo wa ukaguzi wa vyakula vilivyoongezwa virutubishi ambapo pamoja na mambo mengine mwongozo huu umeainisha taratibu za kufuata katika udhibiti wa vyakula vilivyoongezwa virutubishi muhimu katika chakula.
Vilevile  alisisitiza kuwa utoaji wa mafunzo kwa wadau kuhusu uhakiki na udhibiti wa ubora na usalama wa vyakula vilivyooongezwa virutubishi kama vile wataalamu kutoka katika viwanda ni muhimu kwa vile vinavyoongeza virutubishi kwenye vyakula.
Katika hatua nyingine, jukumu jinguine  la TFDA ni kusambaza vitendea kazi vinavyotumika katika uhakiki na udhibiti wa ubora na usalama wa vyakula na kusimamia utekelezaji wa kanuni za uongezaji wa virutubisho kwenye vyakula.
Aidha, Serikali kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii inafanya majaribio katika Halmashauri 6 za Mikoa ya Iringa, Kilolo, Iringa Vijijini, Njombe, Arusha, Karatu, Meru na Monduli ambapo kwa upande wa mafuta ya kula majaribio yanafanyika katika Mikoa ya Manyara, Singida na Dodoma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Hapa ndipo pa kuwa makini sana, kwa faida yetu na ya vizazi vijavyo (in fact ni sisi tutakapurudi katika nafsi tofauti). Ukisikia mbegu imeongezwa virutubisho kwa njia ya mahabara, jua huo ndio mwanzo wa kuongeza kansa mwilini mwako ukila chakula cha aina hiyo!

    Mrutubishaji mkuu ni mwenyewe aliyeumba! Ukiitunza ardhi, ukaijali bila kuimwagiamwagia takataka, bila kuchafua hewa na mvua, hakika utapata mazao yenye virutubisho vya kutosha kukufanya uendelee kuishi kwa afya, bila ya kuwa na spana mkononi!

    ReplyDelete
  2. virutubisho ni kuongeza vitamin na madini kwenye chakula ili kuboresha lishe hii aina shida. Hii inatofautiana na kubadili kiini cha mmea.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...