Rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kwenye Hoteli ya Serena Dar es Salaam jana jioni wakati akitoa taarifa ya kumfuta kazi kocha aliyekuwa akiinoa timu hiyo,Zdravko Logarusic 'Loga' (hayupo pichani). Wengine pichani ni Wajumbe wa Kamati ya Utendaji wa Simba, Collin Frisch na Saidi Tully.
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa Klabu ya Simba, Collin Frisch (kulia), akimsindikiza kwenda kupanda gari kocha wa timu hiyo Zdravko Logarusic 'Loga', wakati wakitoka katika Hoteli ya Serena Dar es Salaam jana jioni, baada ya kutimuliwa kuifundisha timu hiyo. Kocha huyo alikuwa na mkataba wa mwaka mmoja wa kuifundisha timu hiyo. 
Kocha akiondoka huku akiwa aamini kilichomtokea.
Gari namba T 853 BGS alilotumia kocha huyo wakati akiondoka katika hoteli hiyo baada ya kutimuliwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Mm nimefurahi kutimuliwa kwake maana alikuwa akiwafokea wachezaji kama watoto wadogo lkn kwa nn mlimpa mkataba wakati alikuwa ana matatizo mengi huyo kocha mmekula hasara ya bure ya kuvunja mkataba

    ReplyDelete
  2. Ajira za Kibongo hasa Timu zetu ni kama kukalia kuti kavu!

    Hivi kweli mnaweza kumtimua Kocha tena wa Kimataifa kwa matoke ya friend match?

    Je, kama angeifunga ile Timu ya Zambia iliyoifunga Msimbazi 3-1 mngemfukuza?

    ReplyDelete
  3. Mmefungwa Simba na Wazambia ktk friend mechi mnamfukuza Kocha je mkija kufungwa na Yanga ktk Ligi Kuu itakuwaje?

    ReplyDelete
  4. hao makocha wa kigeni hawana utaalamu wowote. tumieni wazalendo, wapeni uhuru wa kufanya kazi, wapeni mshahara mzuri muone kama hawatafanya mabo mazuri sana

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...