Rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kwenye Hoteli ya Serena Dar es Salaam jana jioni wakati akitoa taarifa ya kumfuta kazi kocha aliyekuwa akiinoa timu hiyo,Zdravko Logarusic 'Loga' (hayupo pichani). Wengine pichani ni Wajumbe wa Kamati ya Utendaji wa Simba, Collin Frisch na Saidi Tully.
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa Klabu ya Simba, Collin Frisch (kulia), akimsindikiza kwenda kupanda gari kocha wa timu hiyo Zdravko Logarusic 'Loga', wakati wakitoka katika Hoteli ya Serena Dar es Salaam jana jioni, baada ya kutimuliwa kuifundisha timu hiyo. Kocha huyo alikuwa na mkataba wa mwaka mmoja wa kuifundisha timu hiyo.
Kocha akiondoka huku akiwa aamini kilichomtokea.
Gari namba T 853 BGS alilotumia kocha huyo wakati akiondoka katika hoteli hiyo baada ya kutimuliwa.
Mm nimefurahi kutimuliwa kwake maana alikuwa akiwafokea wachezaji kama watoto wadogo lkn kwa nn mlimpa mkataba wakati alikuwa ana matatizo mengi huyo kocha mmekula hasara ya bure ya kuvunja mkataba
ReplyDeleteAjira za Kibongo hasa Timu zetu ni kama kukalia kuti kavu!
ReplyDeleteHivi kweli mnaweza kumtimua Kocha tena wa Kimataifa kwa matoke ya friend match?
Je, kama angeifunga ile Timu ya Zambia iliyoifunga Msimbazi 3-1 mngemfukuza?
Mmefungwa Simba na Wazambia ktk friend mechi mnamfukuza Kocha je mkija kufungwa na Yanga ktk Ligi Kuu itakuwaje?
ReplyDeletehao makocha wa kigeni hawana utaalamu wowote. tumieni wazalendo, wapeni uhuru wa kufanya kazi, wapeni mshahara mzuri muone kama hawatafanya mabo mazuri sana
ReplyDelete