Mkulima
(wa pili kulia) wa Shayiri katika mashamba ya Monduli Juu, wilayani
Monduli mkoani Arusha akiendelea na uvunaji wa Shayiri kwa kutumia
mashine ya kisasa ambapo wameweza kuvuna hadi gunia 1o kwa hekari moja.
Wakulima wa Monduli Juu wameanza kuvuna mazao yao, baada ya kuwezeshwa
na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) iliyowapatia mafunzo, mikopo ya mbolea
na dawa. Pia shayiri hiyo hununuliwa na TBL kwa ajili ya kutengenezea
kimea katika kiwanda kilichopo Moshi, mkoani Kilimanjaro.
Afisa Ugani wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Kanda ya Monduli Juu na West Kilimanjaro, Editha Temu akipima kuangalia ubora wa Shayiri iliyoanza kuvunwa katika mashamba ya Monduli Juu. Kushoto ni ni Mwenyekiti wa wakulima wa Shayiri Monduli Juu Bariki Kivuyo.
Mkulima wa Shayiri Goigoi Kivuyo akionyesha sehemu ya shamba linalotarajiwa kuvunwa Shayiri eneo la Monduli Juu, wilayani Monduli mkoani Arusha, baada ya kulima kwa kufuata maelekezo na mkopo wa mbegu na dawa kutoka Kampuni ya TBL
: Mkulima wa mfano Mepoloo Lolosi aliyelima hekari 180 za Shayiri katika eneo la Monduli Juu wilayani Monduli, mkulima huyo alikuwa akionyesha baadhi ya zana za kilimo ambazo aliwezeshwa kuzipata kwa njia ya mkopo ili kufikia malengo yake ya kulima kisasa. Tayari amekwisha kumaliza kuzilipia zana hizo pamoja na nyingine.
Meneja wa Barley kutoka Kiwanda cha Bia nchini (TBL) Dk. Bennie Basson akiwaonyesha waandishi wa habari hawao pichani namna Kampuni hiyo inavyowawezesha wakulima wa Shayiri katika kulima kilimo bora chenye tija.

Barley kutengeneza ulevi...tulewe..wapate faida wawekezaji eti wanatozwa kodi...kodi gani; uduchu!
ReplyDeleteAfadhali wanelima ngano!
Mfano mzuri wa kufanikisha KILIMO kwanza kuanzia mbegu, ukulima wa kisasa, pembejeo na soko la uhakika.
ReplyDeleteSerikali kuu, wizara ya kilimo, serikali za mitaa na wadau mbalimbali wanaweza kujifunza mengi toka ushirikiano wa mafanikio wa TBL na wakulima wa shairi na kufanya mapinduzi ktk kilimo cha chakula na matunda.
Hapa hakuna haja ya kwenda nje ya nchi kujifunza bali waende Monduli kuangalia wakulima na TBL wamefanikiwa vipi ktk KILIMO KWANZA kwa vitendo viletavyo manufaa kwa wadau wote.
Mdau
Christos Papachristou
Diaspora.
Safi sana TBL hivi ndivyo tunavyoweza saidia jamii kupambana na umaskini kwa kuwawezesha kulima mazao ya biashara lakini wakiwa na uhakika wa masoko
ReplyDeleteHongera Afisa Ugani kwenye hiyo picha Bi Editha Temu....tunahitaji wataalamu wazalendo kama wewe mnaopambana hapo mlipo na mkiwa tayari kusaidia jamii