Mtuhumiwa Abdul Ghan Peer Bux.

 Imeelezwa kwamba Wapakistani wawili, Abdul Ghan Peer Bux na Shahbaz Malk (pichani) waliokamatwa  wakiwa  na  Watanzania  wanaotuhumiwa kwa kukutwa  na  madawa ya kulevya wametoroka nchini. 

Watuhumiwa hao walikamatwa Februari 21, 2011wakiwa na madawa ya kulevya yenye thamani ya  shilingi  bilioni 6.2,  Mbezi Beach  maeneo ya  Jogoo  jijini Dar sa Salaam.Habari za uchunguzi ndani ya Mahakama Kuu zinasema kuwa, Jaji Grace Mwakipesile anayesikiliza kesi  hiyo  inayotarajiwa kuendelea kusikilizwa kesho Jumatano, ametoa amri ya kukamatwa  kwa  watuhumiwa  hao. 
Kesi hiyo ambayo ilisikilizwa mahakamani hapo Julai 4, mwaka huu ilidaiwa kuwa Wapakistani hao walikamatwa  na  kikosi  kazi  cha  kuzuia na kupambana na madawa  ya kulevya kisha kudhaminiwa lakini wametoweka bila kuhudhuria mahakamani hata siku moja.

Mtuhumiwa Shahbaz Malk. 

Imeelezwa kuwa, baada ya watuhumiwa hao kudhaminiwa na wadhimini wawili, Julai 4, mwaka mahakama iliambiwa kuwa wadhamini hao wamefariki dunia. Hata hivyo, jaji anayesikiliza kesi hiyo aliwaagiza ndugu waliotoa taarifa hiyo kupeleka cheti halisi cha kifo kesho na watuhumiwa wahudhurie mahakamani  hapo.
Madawa ya kulevya yaliyokamatwa na watuhumiwa
 hao yenye thamani ya  shilingi  bilioni 6.2.

Watanzania waliokamatwa na Wapakistani hao waliachiwa huru baada ya kulipa dhamana ya shilingi 10,000,000 ambapo wadhamini wao ni Raza Hussein Kanji ambaye alipewa stakabadhi namba 3406367 na Nazar Mohamed Nurd alikatiwa yenye namba 3406355.
Kamanda wa Kupambana na Kudhibiti 
Madawa ya Kulevya nchini, Godfrey Nzowa.

 Februari 21, 2011 polisi chini ya kamanda wao, Godfrey Nzowa waliwakamata Wapakistani hao wakiwa na Watanzania wawili, William Chonde na Kambi Zuberi ambao wapo nje kwa dhamana wakituhumiwa kukutwa na madawa ya kulevya yenye thamani ya shilingi bilioni 6.2.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. wametoroka; wameenda wapi?hii kiboko. hao tu ndiyo wametoroka; te te te te ...

    ReplyDelete
  2. Only in tanzania,6b drug offense gets bail and now we r told people who bailed these criminals are dead? Chances r the these bail people dont exist, not possible that two people to die,its either be homicide or they didnt exist

    ReplyDelete
  3. Ajabu kweli kweli

    ReplyDelete
  4. Ni nchi gani dunia ya leo ambayo mtuhumiwa wa madawa ya kulevya anwekewa dhamana?I dont think we are at all sincere katika kufight hili janga..

    ReplyDelete
  5. hivi cha kushangaza ni hiki how can those people be bailed wakati offences of the like hazinaga dhamana????

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...