Mtuhumiwa Abdul Ghan Peer Bux.
Imeelezwa kwamba Wapakistani wawili, Abdul Ghan Peer Bux na Shahbaz Malk (pichani) waliokamatwa wakiwa na Watanzania wanaotuhumiwa kwa kukutwa na madawa ya kulevya wametoroka nchini.
Watuhumiwa hao walikamatwa Februari 21, 2011wakiwa na madawa ya kulevya yenye thamani ya shilingi bilioni 6.2, Mbezi Beach maeneo ya Jogoo jijini Dar sa Salaam.Habari za uchunguzi ndani ya Mahakama Kuu zinasema kuwa, Jaji Grace Mwakipesile anayesikiliza kesi hiyo inayotarajiwa kuendelea kusikilizwa kesho Jumatano, ametoa amri ya kukamatwa kwa watuhumiwa hao.
Kesi hiyo ambayo ilisikilizwa mahakamani hapo Julai 4, mwaka huu ilidaiwa kuwa Wapakistani hao walikamatwa na kikosi kazi cha kuzuia na kupambana na madawa ya kulevya kisha kudhaminiwa lakini wametoweka bila kuhudhuria mahakamani hata siku moja.
Mtuhumiwa Shahbaz Malk.
Imeelezwa kuwa, baada ya watuhumiwa hao kudhaminiwa na wadhimini wawili, Julai 4, mwaka mahakama iliambiwa kuwa wadhamini hao wamefariki dunia. Hata hivyo, jaji anayesikiliza kesi hiyo aliwaagiza ndugu waliotoa taarifa hiyo kupeleka cheti halisi cha kifo kesho na watuhumiwa wahudhurie mahakamani hapo.
Madawa ya kulevya yaliyokamatwa na watuhumiwa
hao yenye thamani ya shilingi bilioni 6.2.
Watanzania waliokamatwa na Wapakistani hao waliachiwa huru baada ya kulipa dhamana ya shilingi 10,000,000 ambapo wadhamini wao ni Raza Hussein Kanji ambaye alipewa stakabadhi namba 3406367 na Nazar Mohamed Nurd alikatiwa yenye namba 3406355.
Kamanda wa Kupambana na Kudhibiti
Madawa ya Kulevya nchini, Godfrey Nzowa.
Februari 21, 2011 polisi chini ya kamanda wao, Godfrey Nzowa waliwakamata Wapakistani hao wakiwa na Watanzania wawili, William Chonde na Kambi Zuberi ambao wapo nje kwa dhamana wakituhumiwa kukutwa na madawa ya kulevya yenye thamani ya shilingi bilioni 6.2.
wametoroka; wameenda wapi?hii kiboko. hao tu ndiyo wametoroka; te te te te ...
ReplyDeleteOnly in tanzania,6b drug offense gets bail and now we r told people who bailed these criminals are dead? Chances r the these bail people dont exist, not possible that two people to die,its either be homicide or they didnt exist
ReplyDeleteAjabu kweli kweli
ReplyDeleteNi nchi gani dunia ya leo ambayo mtuhumiwa wa madawa ya kulevya anwekewa dhamana?I dont think we are at all sincere katika kufight hili janga..
ReplyDeletehivi cha kushangaza ni hiki how can those people be bailed wakati offences of the like hazinaga dhamana????
ReplyDelete