Ajali nyingine mbaya:Basi la Abiria linalofanya safari zake kati ya Dar es Salaam - Tabora limepata ajali mbaya sana mchana huu katika eneo la Kiegeya,Gairo na kupelekea zaidi ya watu wanne kupoteza maisha huku wengine wakiwa wamejeruhiwa vibaya sana.Ni majonzi makubwa yametawala katika eneo hilo hivi sasa,huku juhudi za kuokoa miili na majeruhi zikiendelea kama inavyoonekana pichani.ni siku tatu tu zimepita toka ajali nyingine mbaya itokee huko Musoma na kupoteza maisha ya zaidi ya Watanzania 35.Ripota wa Globu ya jamii yupo eneo la tukio hivi sasa na taarifa kamili itawajia baadae kidogo.
Home
Unlabelled
Breaking Nyuzzzzzzz....: ajali nyingine mbaya yatokea Gairo mchana huu,zaidi ya watu wanne wanasadikiwa kupoteza maisha
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
inna lillah wa inna ilayhi rajiun
ReplyDeleteEvery question has an answer, every problem has a solution. Often the answer or the solution may be difficult or unknown, but it is there.Now these nasty Bongo accidents must have a solution, there must be an answer as to why they devastate the people.The accidents are eating up people like some monsters. The nation must arm and fight this demon.How? Lets hear what the Umma says,lets hear the voices of the people.
ReplyDeleteSerikali yafungieni hayo mabasi bila ya hivyo watu watakufa kila siku, hawa madereva hawana ujuzi, leteni madereva kutoka nje ambao wamepitia mafunzo ya udereva, hawa wa hapa kwetu hawana ujuzi wowote, kazi yao ni kutoa rushwa uli wapate reseni
ReplyDeleteRatiba za mabasi zirudishwwe and VIROBA, VIROBA VIROBA vichunguzwe!!!!
ReplyDeleteBadala ya kuwa na Polisi wengi barabarani wakiwa na tochi ambazo hazitusaidii, ni bora wawe na mitambo ya kipima kiwango cha ulevi. Utaona dereva anakunywa maji kumbe yamechangaywa na viroba, gongo, Ooh, matokeo ndio haya!!!
Niliandika comments zangu kuwa angalau rais atakuwa akituma rambirambi angalau mara mbili kwa wiki sasa haijapita hata siku mbili tayari rambi rambi nyingine. KAMA POLISI NA SERIKALI ZISIPOKUWA MAKINI NA HAYA MAMBO YA UDHIBITI WA MADEREVA NA MABASI MABOVU....HILI TATIZO HALITAISHI. SERIKALI ITAMKE AJALI KUWA NI JANGA LA TAIFA NA WALE WAHUSIKA WOTE WATAKAOZEMBEA WACHUKULIWE HATUA KALI NA BILA YA KUONEWA HURUMA.......VINGINEVYO HAYA YANAYOTOKEA YATAENDELEA KUTOKEA KWA SABABU YA UZEMBE WA WATU WACHACHE.
ReplyDeletePoleni wafiwa, poleni sana. Tunawaombea sana tu. Naomba tena ni geuzi kibao kwa ndugu zangu wa jamii hii. Ni ombi sasa. Kwanza tunajua mabasi yanayopata pata ajali katika kila mikoa, jiji. Mji. Na tunawafahamu madereva kichaa. Kama mtu unajua kuweka message kwenye mtandao hata kama ni picha ya dereva huyo, labda tuseme umenusurika toa picha yake na eleza mji na mkasa wa safari, onyo liwe kuwa dereva fulani ni hatari. Utakuwa umeokoa wengi na pia wengi watajitokeza kukubaliana na wewe. Tukiwajua hawa madereva na kuwa tangaza matajiri watalazimika kuto wajiri. Hili nalo lita saidia sana jamii. Mimi nimeanza na aina moja la kutatua tatizo hili bila kumnyooshea kidole mtu yeyote. Naomba wengine tujitokeze na masuluhisho. Kila mtu anaweza kuuokoa maisha ya wengine kama atapenda na kuamua kufanya hivyo. Wengi wanapanda basi wakiamini watafika salaama,laiti wangejua ni kampuni lipi lenye usalaama au madereva wapi wazuri basi wange kua huru kuchagua wata safiri vipi. Najua pia kila mtu akitoa wazo zuri itasaidia tukitekeza hayo mawazo, na pia nafahamu wachache watasimama na kuikashif kauli hiyo nzuri. Kauli nzuri ikipingwa basi wale ambao walikuwa tayari kujaribu hilo zoezi watavunjika moyo. Hivyo basi naomba tusivunjane moyo badala yake tufanye zoezi hili huku serikali na vyombo vya usalaama vikifikiria jinsi gani watalishughulikia tatizo hili sugu. Tuokokoane kwa kusaidiana.
ReplyDeleteWATANZANIA ACHENI KUUA MAALBINO. MNAWAUA MAALBINO WASIO NA HATIA SASA KILIO KIMEHAMIA KWA WOTE.
ReplyDeleteTUJICHUNGUZE ISIJE KUWA NI LAANA YA KUUA MAALBINO.
MCHUNGAJI
Ivi kwanini huko home ikitokea ajari ya gari....mabaki ya gari hua kama yai lilioanguka????si chuma wala bati yaani vyote nyang'anyang'a.
ReplyDeletePoleni wafiwa wote. Marehemu wote wapumzike kwa Amani. Amen. Inasikitisha sana nchi yetu ni maskini sana na uzembe wa madereva wanatuongezea vilema sana nani atawahudumia?
ReplyDeleteMungu tusaidie. Watanzania wote wa ndani na nje ya nchi inabidi tukemee vikali na wahusika wachukuliwe hatua kali za kisheria.
Polisi waache hongo!! Haya yote yanatokana na polisi kula rushwa. Sheria zipo hazifuatwi tu.
ReplyDeletenyie mnaajili polisi wa la saba au form four failure mnategemea nini? kazi yao kukusanya kodi binafsi.
ReplyDelete