Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Tanzania watatu kutoka kulia Akiwa katika Picha ya pamoja Mara baada ya chakula cha Jioni kilichoandaliwa kwa heshima ya kutambua na kuthamini mchango wa Rais na Mwanzilishi wa Taasisi ya Kimataifa inayoshughulika na masuala ya Wafungwa inayojulikana kwa jina la Prisons Fellowship International bwana Gordon Loux wa pili kutoka kulia.Hafla hiyo ilifanyika katika Hotel ya Radisson Blu Mjini Lusaka tarehe 25 Septemba,2014 siku moja Kabla ya Maadhimisho ya Magereza Day ili kutambua Mchango wa Taasisi hiyo kwa Magereza Zambia.Wanne kutoka kulia ni Bi Maureen Mwanawasa mjane wa aliyekuwa Rais wa Zambia Mh.Levy Mwanawasa.Wa pili Kutoka kushoto katika Picha ni Kamishna Percy K Chato Mkuu wa Magereza Nchini Zambia na watatu kutoka kushoto ni Kamishna Jenerali Raphael Tuhafeni Hamunyela Mkuu wa Magereza Nchini Namibia.Na wa kwanza kutoka kushoto ni Bi Ireen Chato Mke wa Kamishna Chato.
Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini Tanzania Bwana John Casmir Minja,akisalimiana na Mgeni Rasmi katika Maadhimisho ya Africa Prisons /Correctional Service Day Zambia.Mheshimiwa Nickson Chilangwa (MP) wakati akiwasili Kwenye Viwanja Vya Chuo Cha Maafisa Magereza Mjini Kabwe Zambia Leo tarehe 26 Septemba,2014.
Kamishna Jenerali wa Magereza Bwana John Casmir Minja akiongozana na wakuu Wengine wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama Nchini Zambia wakielekea Kwenye jukwaa kuu Kabla ya kuanza kwa ratiba.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...