Shirika lisilo la kiserikali la EGPAF limekabidhi vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi 25 milioni kwa hospitali ya wilaya ya Kilwa mkoani Lindi. 

Halfla ya kukabidhi vifaa hivyo vitakavyotumika katika uchunguzi wa awali wa tatizo la saratani ya mlango wa kizazi kwa akinamama ilifanyika jana katika mji wa Kilwa kivinje.

Akikabidhi vifaa hivyo ikiwamo mashine maalum ya kuchunguzia ili kutambua dalili za awali za ugonjwa huo mratibu wa afya,uzazi na jinsia wa shirika hilo,Angasyege Kibona.Alisema katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita,shirika hilo lilibaini ongezeko la akinamama wenye dalili za awali za saratani ya mlango wa kizazi mkoani Lindi na Tanzania kwa jumla.

Kibona alisema hadi kufikia mwezi juni mwaka huu katika hospitali ya mkoa wa Lindi jumla ya wanawake 350 walipatiwa huduma ya upimaji na ugunduzi wa dalili za awali za saratani ya mlango wa kizazi.Ambapo wanawake 17 walikuwa wanaishi na virusi vya UKIMWI(VVU) na 14 walibainika kuwa na dalili za awali za ugonjwa huo.

Mratibu huyo aliongeza kusema kuwa katika kipindi hicho hospitali hiyo iliwapatia rufaa wanawake watatu kwenda katika hospitali ya ocean road jini Dar es Salaam kwa matibabu zaidi.
Mratibu wa Afya,Uzazi na Jinsia wa Shirika la EGPAF,Angasyege Kibona akimueleza jambo Mkuu Wa wilaya ya Kilwa mkoani Lindi,Mh. Abdallah Ulega wahati wa hafla ya kukabidhiana vifaa tiba vitakavyotumika katika uchunguzi wa awali wa tatizo la saratani ya mlango wa kizazi kwa akinamama ilifanyika jana katika mji wa Kilwa Kivinje.
Mkuu wa Wilaya,Mh. Abdallah Ulega akitoa neno la shukran kwa shirika la EGPAF kwa msaada huo utakaosaidia kupunguza vifo vya akina mama wanaopatwa na tatizo la kansa ya shingo ya kizazi wilayani humo.
Mkuu Wa wilaya ya Kilwa mkoani Lindi,Mh. Abdallah Ulega (kushoto) akikabidhi kwa Mganga mkuu wa wilaya hiyo,Dkt. Peter Nsanya baadhi ya vifaa vilivyotolewa na shirika la EGPAF.
Baadhi ya Wauguzi wa Hopitali ya Wilaya ya Kilwa wakiwa kwenye shughuli hiyo ya makabidhiano ya vifaa vya matibabu.
Baadhi ya vifaa hivyo.
Mkuu Wa wilaya ya Kilwa mkoani Lindi,Mh. Abdallah Ulega (kushoto) akiwa na Mganga mkuu wa wilaya hiyo,Dkt. Peter Nsanya wakibadilishana mawazo Mara baada ya kuwasili katika hospital ya kinyonga kupokea msaada wa vifaa Tiba toka EGPAF.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...