Kuna masamalia mwema ametuma Wheelchair kwa Scholastica Mhagama (76)  mwenye ulemavu wa viungo anayeishi pekee yake katika kibanda kilichoezekwa kwa nyasi.
Bibi huyo mkazi wa Kijiji cha Lundusi Kata ya Peramiho wilayani Songea Mkoa wa Ruvuma, Msamalia huyu kutoka Maryland Marekani anaitwa Joyce Rwehumbiza aliguswa na stori iliyotoka Globu ya Jamii (BOFYA HAPA)  na baadaye kuandikwa na magazeti kadhaa  na kuweka mawasiliano ya   albano.midelo@gmail.com, 0688551355 iliyobeba kichwa cha habari "Bibi ajitengenezea jeneza baada ya kuchoshwa na dhiki" 
Joyce Rwehumbiza ameishatuma Wheelchair hiyo inafika Dar es Salaam leo Ahamisi Sept 11, 2014 na amejaribu kuwasiliana na mwandishi wa hii stori lakini hakuweza kumpata ameomba tafadhali Albano Midelo awasiliane na namba 0765 835722 wheelchair itafikia hapo na ameombwa afanye haraka kwani baada ya siku 2 huyu mama anatarajiwa kusafiri.
Bibi Scholastica Mhagama akiwa amejitengenezea jeneza lake

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. the best investment in this world is HELP.BE BLESSED ndugu kwa moyo wako wa uzalendo,na sisi tutaiga mfano wako na wa wengine wote wenye mapenzi mema,GOD BLESS YOU.

    ReplyDelete
  2. Dear Michuzi. Tumshukuru sana Mdau mwenzenu huyu kwa moyo wake wa huruma, hatumvunji moyo lakini nadhani huyu mama hiki kiti hana cha kukifanya, coz hana muendeshaji, kwa yeye pekee itamchukuwa muda kukiahamu na kukielewa kukiendesha pekee hiki kiti. The only support she needs ni kutolewa kule kijijini akaletwa kunako watu. ANAHITAJI MSAADA WA KIBINAADAMU

    ReplyDelete
  3. Msamaria huyo mwanadiaspora aliye ughaibuni abarikiwe mpaka ashangae. Jamani mwingine wa hapa bongo je, kutoka Songea viongozi wananchi mko wapi? tujitokeze kuondoa nyasi kuweka mabati, kuondoa ukuta wa udongo kuweka tofali, mwingine aweke solar, mwingine tanki la simtanki, masufuria na vyombo vya kisasa kuliko hivyo kwenye picha, radio je? simu je yaushukuru wasamaria ikiwa na salio la kutoosha?. Kutoa ni moyo siyo utajiri. Sasa mbona contact hapatikani?

    ReplyDelete
  4. Mdau wa pili, tatizo ni kwamba tukikimbia wote vijijini nani atapaboresha, kama ni issue ya repair mafundi wa baiskeli wanaweza kurepair.. Ukweli ni kwamba maisha ya mjini hayakaliwi tu hivi hivi lazima uwe na uwezo wa kulipa bili za nyumba na mahitaji mengineyo. Unapoboresha mazingira vijijini unahamasisha wakazi wa kuko pia kuishi vizuri.

    ReplyDelete
  5. Mwenyeez Mungu amjaze kila la kheri na ampe saba wa sabiini In Sha Allah, msamaria huyo mwema kwa kuguswa na kuingiwa na huruma na hatimae kujitolea msaada wake huo. Pia nawashkuru sana wanakhabari waliohusika katika kulifatilia suala hili zima la Bibi yetu Bi Scholastica baada ya kubaini hapo alipokuwa aikiishi, hali yake ya kiafya na mazingira magumu aliyokuwa akiishi kwa jumla na kuweza kutukhabariisha kupitia hapa kwenye blogu hii na khatma yako waliojaaliwa na chochote kila cha kutowa ili kumsaidia Bibi yetu huyo Bi Scholastica, basi wameonyesha huruma na upendo wao wa dhati kwa kutowa msaada mithili ya huo wa hiyo 'Wheelchair', pia naamini Bibi Scholastica ataendelea kuangaliwa kwa ukaribu zaidi na kuishi katika maisha bora na salama khasa tukizingatia umri alionao na hali yake halisi ya kiafya kwa jumla. In Sha Allah, MOLA akulinde na kukujaalia umri mrefu Bibi yetu Bi Scholastica, pia atujaaliye nasi sote moyo wa kujali, upendo na huruma kwa wazee mithili ya Bibi Scholastica, wenye kuishi katika mazingira yanayohitaji huduma na hata misaada mithili hiyo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...