Na John Gagarini, Kibaha.

MKAZI wa Kijiji cha Bupu kata ya Bupu Tarafa ya Mkamba wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani Forodesi Ntabegera (30) ameuwawa kwa kubakwa kisha kunyongwa na watu wasiojulikana kisha mwili wake kutupwa kichakani.

Kwa mujibu wa taarifa ziliotolewa na kaimu kamanda wa polisi mkoani Pwani Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani humo Mrakibu Msaidizi wa Polisi (SSP) Athuman Mwambalaswa Marehemu kuwa marehemu alinyongwa na watu hao kwa kutumia kitenge chake alichokuwa amekivaa.

Kamanda Mwambalaswa alisema kuwa tukio hilo lilitokea Septemba 9 mwaka huu majira ya saa 8:00 mchana baada ya wakazi wa kijiji hicho kufanya msako wa kumtafuta marehemu ambaye alipotea Septemba 8.

“Baada ya msako huo kufanyika mwili wa marehemu ulikutwa kwenye kichaka umbali wa mita 30 kutoka barabarani ambapo mwili wake ulimwagiwa unga sehemu za kichwani na mgongoni,” alisema Kamanda Mwambalaswa.

Alisema watu hao walitumia mfuko wa salfeti aliokuwa amebebea unga aliotoka kuusaga mashine, kumvisha miguuni kisha mwili wake waliulaza kifudifudi.

Aidha alisema kuwa taarifa za kupotea marehemu zilitolewa na kituo cha polisi Kimazinchana na mwenyekiti wa Kijiji cha Bupu Kasimu Kambangwa walioongozana na watoto wa marehemu ambao walidai mama yao alitoweka baada ya kuaga kuwa anakwenda kusaga na hakuonekana tena hadi mwili wake ulipokutwa kwenye eneo hilo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Kwenye watu mia binadamu mmoja. I never knew the woman, but I have tears in my eyes,huyu pengine alikuwa ni mke wa mtu na mwenye watoto wake, hajui hili wala lile anatoka kusaga mahindi kwa ajili ya ugali ailishe familia yake, halafu hii MIFEDHULI isiyo na ubinadamu immembaka na baadae kumnyonga,tunakoenda kubaya. Hopefully hii miuaji itashikwa na inyongwe mpake ife.
    RIP Forodesi, so very sad.

    ReplyDelete
  2. TWILA KAMBANGWASeptember 10, 2014

    RIP ma wa watu inauma sana, wakikamatwa wanyongwe mpaka wafe

    ReplyDelete
  3. Dah kwa kweli inauma sana japo simjui...Hii inatufanya sote tuwe waoga tukiona wanaume wkt unatembea mwenyewe...Watu wamekuwa hawana utu...Mungu awalaani kwa kitendo walichokifanya na wakamatwe

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...