Kutoka kushoto ni Gwiji wa muziki wa dansi nchini Mzee Kassim Mapili
akiwa amekaa kwenye kitanda cha hospitali ya Taifa Muhimbili kushoto ni
Rais wa Shirikisho la Muziki wa Dansi Tanzania Addo November
alipokwenda kumjulia hali leo asubuhi hospitalini hapo.
NA BONGOWEEKEND BLOGSPOT.COM
NA BONGOWEEKEND BLOGSPOT.COM
HALI ya mwanamuziki nguli Kassim Mapili aliyelazwa katika
Hospitali ya Taifa Muhimbili katika kitengo cha moyo inaendelea
vizuri imehafamika.
Mapili ambaye awali alilazwa katika Hopitali ya Mwananyamala kutokana na kusumbuliwa na maradhi ya mapafu kujaa maji pamoja na moyo kujaa maji ambako alilazwa kwa
muda wa siku nne kabla ya kuhamishiwa katika Hospitali ya Muhimbili juzi mchana.
Hayo yalisemwa leo na Rais wa Shirikisho la Muziki Addo November ambaye aliefika hospitalini hapo mapema asubuhi
kumjulia hali Mapili ambapo alikiri kuwa
amelazwa katika wodi namba moja katika Taasisi ya Moyo baada ya kutolewa katika wodi ya uangalizi maalumu (ICU),
Muhimbili.
Aidha November ametoa rai kwa wadau na wanamuziki viongozi
mbalimbali kujitokeza kwa wingi
kwenda kumjulia hali gwiji huyo wa muziki ikiwa ni sehemu ya kumpa faraja kwa
ujumla.
“Mzee wetu anaumwa
sana na amevimba sana miguu hivyo ni wajibu wa kila mmoja wetu kutoa msaada wa
hali na mali” alisema November.
Wakati Mapili akiwa amelazwa mama yake mzazi aliyetajwa kwa jina la Hajena Mussa Mchikita amefariki usiku wa juzi nyumbani
kwake Nachingwea na atazikwa leo mkoani Songea alisema November .
Mapili alitamba na nyimbo
za ‘Rangi ya Chungwa’, ‘Mayasa’ ambao aliuimba na Marehemu TX Moshi William
enzi za uhai wake na kutamba vilivyo
katika miaka ya 1980.
Mzee Kassim Mapili tunakuombea afya njema Mwenyezi Mungu akuvue ugonjwa huo na kukupa afya zaidi,wewe ni mmoja wa wakongwe adimu katika historia ya muziki wa dansi Tanzania.
ReplyDeleteTunakuombea Afya njema Mwenyezi Mungu akufanyie wepesi upone kwa haraka baba.
Wadau
FFU-Ughaibuni
www.ngoma-africa.com