Stuttgart,Ujerumani,
Usiku wa Jumamosi ya Tarehe  30.Augost 2014, majira ya saa 10 alfajiri
Mwanamuziki nyota wa Bongo Flaver  Nasib Abdul aka Diamond Platnumz alijikuta katika hali ya hatari hadi kuokolewa na Polisi mjini Stuttgart,Ujerumani,baada ya washabiki waliokuwa na hasira kuchoka kusubiri show.

Washabiki hao waliokuwa wamelipa ticket euro 25 kwa kiingilio waliahidiwa kuwa show ingeanza saa 4.00 usiku,lakini walijikuta wakisubiri hadi majira ya saa 10 usiku au alfajiri ndipo mwanamuziki Diamond alipoletwa jukwaani na promota wake Mr.Awin Williams Akipomiemie raia wa Nigeria anajiita kama Britts Event.

Hapo ndipo washabiki hao walipoona kuwa hawakutendewa haki walianza kurusha chupa na kutaka kumvamia mwanamuziki  Diamond na promota wake,
Kilichowakera zaidi washabiki ni pamoja na vyombo vibovu vilivyofungwa katika ukumbi huo kitu ambacho kiliwafanya washabiki kuvunja hadi vyombo vya muziki
ma-Djs walishambuliwa na wapo Hosptalini kwa sasa.

Moja wa Djs hao alipoteza Lap top yake ,mwanadada DJ  Flor alipatwa shock mstuko wa moyo na kukimbizwa hosptali, washabiki hao walimpa kipigo  DJ Drazee naye yupo hoi hospatal. 

Polisi nchini Ujerumani wamesema tukio hili la aibu halijawahi kutokea,kwani msanii kuchelewa kufika jukwaani kwa ujerumani ni kitu cha hatari sana,kwani washabiki wa ujerumani wanaheshimu sana muda wao.

mpaka sasa polisi wanamsaka mwandaaji wa onyesho hilo na wamesema kuwa
wanachunguza thamani ya hasara iliyosababishwa na ghasia hizo na pia itamfungulia mashataka promoter huyo raia wa Nigeria,ambaye pia anachunguzwa kwa kusemekana anajihusisha na mtandao fulani wa biashara.
Hivi ndivyo ukumbi huo ulivyokuwqa baada ya tafrani hiyo.

Magazeti ya Stuttgart; yameandika "Washabiki wana hasira nawe DIAMOND"  link:

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Ni nini hasa shida ya ku keep time?

    ReplyDelete
  2. Diamond ulizoea mchekea wa TZ...Wenzetu wana mipangilio ya maisha hawakurupuki...Nawewe unapaswa kuwa mstaarabu. Umetembelea nchi nyingi za ulaya inbidi ubadirike.. Tabia za kwenu bongo ukizipeleka kwa watasha utakisikia.

    Ukienda Rome ishi kama wati wa Rome

    ReplyDelete
  3. Naona dogo anapeleka mambo yake ya Tandale. Nadhani kapata fundisho. Na, tunasubiri uchunguzi wa polisi kuhusu promota wake kuwa anajihusisha na biashara ya sembe.

    ReplyDelete
  4. Time is money. Take it very serious.

    ReplyDelete
  5. Jamani Wewe Diamond sasa ni mwanamuziki mkubwa angalia sana mapromota unaonfanya nao kazi. Hawa mapopo wengi ni matapeli tu. Pole sana, jina limeshachafuliwa.

    ReplyDelete
  6. Diamond tafuta promotor wa Tanzania. Chezea mapopo kama hawatakuaharibia biashara.

    ReplyDelete
  7. Anajifanya shooo off sana wangemwacja apigwe barabara angetia akili

    ReplyDelete
  8. Safi sana fundisho la mda lichukuriwe seriously hasa hawa wanyanje wanava nguo za kubana na viatu vyaajabu wanajifanya mapromo zuga wako wengi.I'm dj sikupenda walicho wafanyia djs they have nothing to do with this show

    ReplyDelete
  9. Please fire your promoter.

    ReplyDelete
  10. Diamond, liwe fundisho kwako. Si ulujua saa fulani unahitajika sehemu fulani, ulipitiwaje hivyo? Saa kumi ? Wewe siyo bongo star ni zaidi ya hapo. Mastaa wengi huanguka kwa sababu ya makosa. Tizama usijeingia ktk huo mkumbo. When Rome act like the Romans.

    ReplyDelete
  11. Watandale ulaya aiweze vipi, brash angalau o level bwana

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...