Shuhuda aliyenusurika kwenye mauaji ya Albino ambaye amekatwa mikono yote miwili, Mariam Stanford akitoa ushuhuda wake na killio chake mbele ya meza na wageni waalikwa waliohudhuria sherehe za maadhimisho ya siku ya kimataifa ya amani iliyofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam kwenye viwanja vya Mnazi mmoja.(Picha na Zainul Mzige wa MOblog).
======= ======= =======
Mwanamke albino Mariam Stanford aliyepoteza mikono yake yote miwili wakati iliponyofolewa na majahili asiowajua Oktona7, 2008 ameitaka serikali kuwanyonga wote wanaopatikana na hatia ya kuua albino nchini.
Alisema hata adhabu ya kifungo cha maisha haiwatoshi kwa jinsi wanavyosababisha maisha ya mashaka na yenye uchungu kwa walemavu wa ngozi. Akiongea kwa uchungu huku hapa na pale akitulia kwa kuzidiwa na machozi kiasi cha kushidwa kuzungumza Stanford ambaye alisema wakati akikatwa mikono yake alikuwa na mimba ya miezi mitano na ambayo ilitoka alisema majahili hao si wa kusamehewa.
Alisema akiwa mama wa familia kitendo cha kumuondolea mikono yake kimemfanya kuwa tegemezi hali ambayo inaongeza maumivu juu ya maumivu ambayo anayo ya kunyanyapaliwa na jamii.
Alisema hayo wakati akitoa ushuhuda katika adhimisho la siku ya amani duniani iliyofanyika kitaifa katika viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam. Alisema japokuwa Tanzania inaelezwa kuwa nchi ya amani wananchi wake wenye ulemavu wa albino hawana amani kutokana na kuwindwa kama digidigi. Alisema kwa sasa Tanzania ni kisiwa cha matatzio kwa kundi hilo ambalo sasa linajificha na wala kutokujua kesho ikoje au siku hiyo ikoje.
Mke wa Balozi wa Uturuki nchini Yesim Davutoglu, akilia kwa uchungu baada ya kusikia shuhuda kutoka kwa mhanga wa mauaji ya Albino aliyekatwa mikono yote miwili, Mariam Stanford (hayupo pichani) ambaye hadi sasa anapewa matunzo na Shirika la Under The Same Sun.
Kwa kweli inasikitisha sana kuona binadamu mmoja badala ya kufanya kazi kujiinua kimaisha anajiona bora kuliko wengine hata kuwa tayari kuua au kuwakata mikono kwa sababu za kishirikina.
ReplyDeleteHajakosea kuomba wahusika wanyongwe, inauma sana, utu na ubinadmu vimekwenda wapi?
DeleteThanks
DeleteNaunga mkono pendekezo la kuuwawa. Katiba mpya inatakiwa ieleze hivyo ili wanaofanya vitendo hivyo wapewe adhabu ya pekee. Hiyo inaweza kusaidia kukomesha matendo hayo.
ReplyDeleteTANZANIA TUNATIA AIBU!!
ReplyDeleteHili swala siyo la kuppuza. Kaka Michuzi hili nalo naomba utupe nafasi yakulijadili. Albino tunateswa kaka tunaomba nafasi tusikike. Tanzania tujumuikekulizungumzia hili swala zito. Yaani jinsi gani kusitisha kukatwa viungo na kuuwawa kikatili.
ReplyDeleteIt is amazing that as a country we have not stood by our Albino family. Yes! After all they are born from non Albino parents AND they give birth non Albino offspring for the most part.
ReplyDeleteIgnorance is the first thing to address! It really is, by making a country wide campaign to say that killing Albinos is incorrect to to keep this conversation open and ongoing would help alot. Coverage of these types of atrocities should be reported more frequently to raise the alert, and to sensitize everyone on a huge wrong done. This is corrupting our peace.
It should be no surprise to villagers or towns as to who is demanding the body parts of an albino. The culprits should be confronted and punished publicly, its a bad addiction to kill.
When a person ceases to be identified as an Albino, but as a living being of a specific family, it shows that society cares, when we label these wonderful family members we have that means at a subtle level as a society we have dis associated ourselves from them, it shows lack of compassion, lack of human ness.
Lets say NO! No Killing or maiming our brothers and sisters. It is not right. Boycott this very act!
Enough is enough!