WASANII TUSIWE WATU KULAUMIWA KILA WAKATI! BALI KUSHAURIWA,
WASANII LAZIMA WAANGALIE KWA MAKINI MIKATABA NA MUDA KUTUMBUIZA
Baada ya vyombo vya habari kuandikia kwa wingi tukio la fujo zilizotokea wikiendi ya 30.Augost 2014 katika show ya mwanamuziki Diamond, Blog ya jamii na timu ya Michuzi Media imefanya juhudi za kutaka kusikia maoni na mtazamo wa mwanamuziki wa Tanzania aliyeupigania muziki wa Tanzania katika soko la ughaibuni kwa miaka 21 si mwingine bali ni Kamanda ras Makunja wa FFU
au Ngoma Africa Band.
Michuzi media ilianza kwa swali ?: Ras Makunja nini mtazamo wako kwa
Yaliyotokea Stuttgart.?
Kamanda Ras Makunja: " Kwanza nianze kwa kuwapa pole wale wote waliopatwa na usumbufu na maumivu yawe ya mwili,hisia au hali kutokana na tukio lile,kwa kweli tuliposikia tulistuka sana sana" ,Ras Makunja alisema.
Kwa kuwa sisi sote tunajua ugumu wa msanii anapokuwa On Tour hususan ugenini ,kuna taarifa za awali ambazo msanii ni vigumu sana kuzipata,taarifa ambazo ,pengine zinaweza kumsaidia msanii kwa namna moja au nyingine,kwa kweli msanii anapokuwa ugenini ni sawa na usiku wa kiza.Ras Makunja alisisitiza
Tunacho shukuru Mungu pamoja na yote yaliyotokea pale hatukusikia kama kuna mtu aliyepoteza uhai,maana uhai ni zawadi ya Mola kwa viumbe wake.
Wito wangu kwa wadau na washabiki kwa kuwa nyinyi ndio ma-boss zetu,na sisi wasanii au wanamuziki ni watumishi wenu,ningewaomba msichoke kuunga mkono mara mnaposikia msanii au mwanamuziki,au bendi inapiga sehemu fulani,Kwa sababu Chereko Chereko na mwenye mwana.
Fujo zilizotokea pale Stuttgart kila moja kasoma katika vyombo vya habari na nyinyi ndio mahakimu,lakini mimi si msemaji wa upande wowote pale bali kama msanii ningeomba msimuhukumu msanii kwa kosa la mtu mwingine.
MICHUZI MEDIA : Unawashauri nini wanamuziki wenzako kutoka nyumbani wanaokuja kutumbuiza ?
Ras Makunja: Ushauri wangu nimeshausema mara nyingi katika vyombo vya habari kuwa, Wasanii wa nyumbani lazima wanapopata mikataba waipeleke kwa mameneja na mwanasheria ili isomwe na kueleweka kipengele kimoja baada ya kimoja mfano: taratibu za malipo cash au? na muda wa kulipwa kabla au baada ya show: Hotel,Bima ,VAT,Ulinzi na Kingine muhimu ambacho mara nyingi ndicho chanzo cha mizozo ni malipo na muda wa kutumbuiza hili lazima liwe wazi tena ndani ya mkataba,Mfano show inaanza saa 4 usiku hadi 7.usiku basi lilwe wazi.
Unajua kuna baadhi ya mapromota wanapenda sana kutufanya wasanii kuwa mashine, mara nyingi wanavunja utaratibu "anakuweka hoteli na yeye anasubiri watu wajae ukumbini au wanunue vinywaji kwanza ,sasa
watu wakishalewa unategemea nini? ni fujo tu lakini kama mkataba unaeleza time ya kutumbuiza na mwisho wa show,ata kama kuna watu wawili msanii anatumbuiza.
"WASANII WA AFRIKA MASHARIKI WAPENDWA SANA ULAYA"
Ras Makunja alisema baada miaka 21 ya kupigania soko na moyo wa wadau na washabiki wa sanaa za Afrika Mashariki sasa sanaa zetu zimeshika soko na baadhi ya wasiopenda maendeleo wanatutazama kwa macho ya makengeza !
Wasanii lazima tuangalie sana sana nani wa kufanya nae kazi,katika music Industry kuna baadhi ya watu wanamfanya msanii ni kipande cha ndimu "anakamua na kutupa ganda"
Msanii anapata tabu kujenga jina kwa miaka,eti promota anataka kulibomoa kwa dakika usipokubaliana na yake,lazima wasanii wajichunge sana.
Wasanii wa Afrika Mashariki tunawapa wakati mgumu wapinzani wetu,na wapinzani wetu wanajua vema kuwa pia sisi ni wakarimu hapo ndipo wanapojaribu kutumaliza na ukarimu wetu.
Nawashauri wasanii wezangu wale wanaokuja ujerumani,kabla hujasafiri jaribu kuwasiliana na umoja wa waTanzania Ujerumani(UTU) email yao hii kamati.utu@googlemail.com ili upate information muhimu,hakuna
atakaye kuingilia katika biashara au mkataba wako lakini ushauri ni muhimu.
Pia lazima tujijue kuwa kwa sasa tunatishia soko na tayali lipo mikononi mwetu kwa maana hii wapinzani wanajaribu kujifanya wao ndio mapromota lazima tujipange na kutambua nani wa kufanya nae kazi na kwa makubaliano yepi.
Habari za uhakika tunazo kuwa mwaka 2015 wasanii wa Afrika Mashariki ndio wanaotakiwa kwa wingi hapa ughaibuni,tumieni nafasi hiyo.
KARIBUNI SANA KATIKA SOKO LA UGHAIBUNI NA MKIPATA NAFASI ZA
KUTUMBUIZA LAZIMA MKAMUE BILA YA HURUMA.
Asanteni, pia nawashukuru sana Michuzi Media kwa kunipa nafasi.
Rasi ushauri wako nimuhimu sana kuzingatiwa. kwa uzoefu wangu,ni hivi tatizo hili alitaisha kwa hizi shoo za uchochoroni za kuwapigia watanzania wakenya na waganda ,nk. kama shoo anazo fanya RAS ZA MATAMASHA YA KUELEWEka sidhani usumbufu kama huu unaweza kutokea.mimi huwa najiuliza kaukumbi kama hako unavyokaona ni promota anaganga njaa tu wapelekeni wasanii wetu kwenye matamasha makubwa ambayo hata mikataba yake ni ya kueleweka. pia sio kama nawasema vibaya wanageria ila chunga sana unapo fanya nao kazi mimi niko huku hawa jamamaa na wengine west afarika nikuwa makini nao . tujifunze wasanii wa bongo, muda sasa umefika kutafuta matamasha makubwa. kaka s
ReplyDeletekamanda mkuu ras makunja asante sana
ReplyDeletekwa ushauri wako kwa hawa vijana wetu wanamuziki chipukizi,kwa weli inasikitisha sana wanapopata nafasi ya kuja ughaibuni lakini wanakuwa wapo gizani bila ya kuwa na information muhimu,wajaribu kuwasiiana na jumuiya za wa TZ za huko.Kamanda asante sana kwa ushauri
kamanda mkuu wa ffu,ushauri wako mzuri umeelemika lakini hawa vijana wenu ni wabishi hawapendi kumshirikisha mtu mtaalam katika shughuli ndio maana yanawakuta mengi
ReplyDeleteusisahau usemi ule wa makaidi afaidi mpaka siku ya Idd
Makunja mbona nyie mpo ndani ya gemu kwa miaka na mnatumbuiza maelfu ya washabiki hatujawai kusikia mmechelewa jukwaani,katika sakata la
ReplyDeleteDiamond lazima kulikuwa kuna ubabaishaji fulani
Promota Britts Event inasemekana ndio zake kila show anayoandaa mwisho wake ni timbwili
ReplyDeleteRas makunja mkuu wa himaya ya viumbe ajabu Anunnaki tunashukuru kwa somo,lakini watoto wenu wa kizazi kipya hawana nidhamu wala utaratibu
ReplyDeletewanapoitwa sehem wao pesa mbele uhai baadaye,sasa katika sakata lile labda watasoma
Bwana kamanda mkuu tumekusikia sisi wadau kila wakati tupo pamoja nanyi wasanii ,tungependa nanyi basi muwe mnawaeleza hao waandaaji wenu kuwa
ReplyDeleteTIME MORE THAN MONEY wakati ni uhai,
tusiwe tunawasubiri kama vie tuna msubiri YESU
kamanda mbona nyie mkienda kwenye show zenu mnawekewa ulinzi mkali! sasa kwa nini Stuttgart pasiwe na ulinzi mambo yamepelekwa kienyeji enyeji
ReplyDeletemkuu makunja mimi nakubaliana nawe
ReplyDeleteukarimu wa wabongo unawapa upenyo wapinzani wetu ,nina wasi wasi labda katika makubaliano ya Diamond na promota mpopo kulikuwa na ukarimu wa kuitana ndugu au brother matokea yake ndio vile
kaka makunja ata ukiwashauri vipi? watoto wenu wa bongo flava ni wabishi wameweka sifa mbele kuliko uhai wao,angalia sasa wanijeria wanavyo waweka kinyumba
ReplyDeletewasanii wa bongo kweli wababaikaji,
ReplyDeletemmekuwa limbukeni wa ajabu angalia mnaijeria anababaikiwa na ndiye mnamwita promota ni ujinga
Kaka Makunja wewe haukuwepo pale,
ReplyDeletemimi nimesafiri na mume wangu na marafiki zangu kutoka wurzburg mpaka Stuttgart kwa ajili ya kuungamkono
tulichoambulia rafiki yangu kapigwa chupa ya mkono,mume wangu kapoteza pochi ni aibu,siendi tena kama muandaaji ni yule mjinga mpopo.
Mdau
Judith Otieno
ujinga tena ni ujinga yaani tulipoteza muda na pesa zetu pale kwa ajili ya kwenda kununua bia mpaka 4.00am please never again
ReplyDeleteJoka kuu kamanda ras makunja mtawala wa himaya ya viumbe wa Anunnaki,tumekuelewa lakini mbona nanyi wasanii wa bongo hambadili tabia zenu ? kila kukichwa ni uhuni tu sasa sisi wadau tutawapa shavu vipi? kwa miradi hii ya kutiana hasara
ReplyDeleteMakunja unajua kinachouma zaidi ni kuona nyinyi wasanii badala kwenda mbele sasa mnashirikiana na watu wanao warudisha nyuma,sasa nani ? mchawi wa kazi zenu kama siyo nyinyi wenyewe! badilikeni
ReplyDelete