Hatimaye Serikali imetimiza ahadi yake mapema leo mara baada ya Kivuko
cha Mv. Kigamboni kuanza rasmi safari zake za usafirishaji.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara
ya Ujenzi Mhandisi Mussa Iyombe wakati akizindua kivuko hicho ambacho
kilikuwa kikikarabatiwa na Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Kikosi cha
Wanamaji.
Mhandisi Iyombe amesema Kivuko hicho ambacho kinategemewa na
wananchi walio wengi waishio Kigamboni na maeneo jirani kimeanza kutoa
huduma zake za usafirishaji ambao ulikuwa umesitishwa kwa muda wa
takribani mwezi mmoja.
“Ile ahadi ya kukikarabati na kukirudisha kivuko cha Mv. Kigamboni
hatimaye leo imetimia na wananchi wamejionea wazi juu ya utendaji na
ufatiliaji wa huduma muhimu kama hizi za vivuko”, alisema Katibu Mkuu
Aidha, Katibu Mkuu amelipongeza Jeshi la Wananchi Tanzania Kikosi cha
Wanamaji kwa uzalendo wao waliouonesha kwa kukamilisha ujenzi huo
kwa gharama nafuu na kwa wakati ili kurejesha huduma za usafirishaji.
Akizungumza kwa niaba ya wakazi wa Kigamboni Bw. Davis Hokororo
ameipongeza Serikali kwa huduma ya ukarabati walioufanya na ameiomba
serikali kuongeza kivuko kingine kikubwa ili kukidhi haja za wakazi wa
Kigamboni na maeneo jirani.
Pia ameiomba Serikali kutokupeleka kivuko cha Mv. Magogoni kwa wakati
huu mpaka kusubiri kukamilika kwa barabara ya Kongowe ili kurahisisha
huduma za usafirishaji kupitia njia ya vivuko na barabara.
Kivuko cha MV KIgamboni kikiwa majini kuelekea eneo la Ferry kwa ajili ya
kuanza kutoa Huduma ya Usafiri.
Abiria wakipakia kwenye Kivuko cha MV Kigamboni mara baada ya kuanza
kufanya kazi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...