Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Bw. Wilman Ndile afungua Warsha ya Siku Mbili Wilayani Mtwara kuhusu “Mpango wa Kujikinga, Kukabiliana na Kuzuia athari za Maafa kwa Wilaya ya Mtwara leo tarehe 26 na 27 Septemba, 2014.

Wakati wa ufunguzi huo Bw. Ndile alisema Mpango huu utasaidia sana pindi maafa yatakapotokea na kuwaomba washiriki wa warsha hiyo kutoka Manispaa na Halmashauri ya Wilaya hiyo kushiriki vema katika mafunzo na kuchangia masuala hayo ili kuweza kukamilisha mpango huo unaoratibiwa na Idara ya Uratibu wa Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu.

Alisema “hatua hizi zimekuwa madhubutu na zitatusaidia sana sisi kama wadau wakubwa wa Maafa katika Halamshauri zetu na Manispaa kwa kuona uzito wa suala la Maafa ni la kila mmoja na sio Ofisi ya Waziri Mkuu ambaye ni mratibu tu wa Maafa” alisisitiza Bw. Ndile.
 Mkuu wa Wilaya ya Mtwara,Wilman Ndile (aliyesimama) akifungua Warsha ya Siku Mbili kuhusu “Mpango wa Kujikinga, Kukabiliana na Kuzuia athari za Maafa kwa Wilaya ya Mtwara leo tarehe 26 na 27 Septemba, 2014.
Mratibu wa Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu Bw. Fanuel Kalugendo akieleza lengo Tathmini ya Viatarishi, Uwezekano wa Kuathirika na Uwezo wa Kukabiliana na Maafa yaani (Risk Vulnerability and Capacity Assessment - RVCA) ya siku mbili tareha 26 na 27 Septemba, 2014 kwa wadau wa Maafa wa Manispaa na Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara.
Washiri wa warsha kuhusu maafa kutoka Manispaa na Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara wakimsikiliza kwa makini Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Bw. Wilman M. Ndile (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa warsha ya Siku mbili inayoratibiwa na Idara ya Uratibu wa Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu kuhusu Tathmini ya Viatarishi, Uwezekano wa Kuathirika na Uwezo wa Kukabiliana na Maafa yaani (Risk Vulnerability and Capacity Assessment - RVCA)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...