Washindi
wa Tuzo za Habari za TANAPA 2013 wakiwa pamoja na Mhariri Mkuu wa Habari
na Matukio wa Channel Afrika ya Shirika la Utangazaji la
Afrika Kusini (SABC) Busi Chaane (wa tatu kushoto) pamoja na Mkuu wa Idhaa
ya Kiswahili ya Channel Afrika ya SABC Mike Arareng (wa kwanza kulia)
walipotembelea studio hizo kwa ziara ya mafunzo.
Washindi
wa Tuzo za Habari za TANAPA 2013. Kutoka kulia ni Vedasto Msungu (ITV),
Gerald Kitabu (The Guardian), David Rwenyagira (Radio Five) na Meneja
Mawasiliano wa TANAPA Pascal Shelutete katika picha ya pamoja katika ofisi
za Shirika la Utangazaji la Afrika Kusini (SABC) jijini Johannesburg.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Jukwaa la Wahariri nchini Afrika Kusini Mathatha Tsedu (mwenye
kofia) akimsikiliza kwa makini Meneja Mawasiliano wa TANAPA Pascal Shelutete
wakati wa ziara ya mafunzo kwa washindi wa Tuzo za Habari za TANAPA 2013 nchini
humo. Baadhi ya washindi hao ni pamoja na Vedasto Msungu kutoka ITV (kulia) na
Gerald Kitab.
Washindi
wa Tuzo za Habari za TANAPA 2013 . Kutoka kulia ni David Rwenyagira (Radio
Five), Vedasto Msungu (ITV), Gerald Kitabu (The Guardian) na Meneja
Mawasiliano wa TANAPA Pascal Shelutete wakiwa nje ya Ofisi za Makao Makuu
ya Jukwaa la Wahariri Afrika Kusini.
Washindi
wa Tuzo za Habari za TANAPA 2013 wakifanya
mahojiano ndani ya Studio za Shirika la Utangazaji la Afrika ya
Kusini (SABC- Channel Afrika).
Kutoka kushoto ni David Rwenyagira (Radio Five), Gerald Kitabu (The Guardian),
Vedasto Msungu (ITV) na Mtayarishaji Vipindi Isaack Khomo.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Jukwaa la Wahariri Afrika Kusini Mathatha Tsedu (wa tatu
kulia) akiwa pamoja na Washindi wa Tuzo za Habari za TANAPA 2013. Kutoka
kushoto ni Gerald Kitabu (The Guardian), Vedasto Msungu (ITV), David
Rwenyagira (Radio Five) na Meneja Mawasiliano wa TANAPA Pascal Shelutete.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...