Waziri  wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe akisalimiana na Balozi wa Marekani nchini, Mhe. Mark Childress alipofika Wizarani kwa ajili ya mazungumzo kuhusu masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Marekani na kukumbuka Wahanga wa tukio la kigaidi lililotokea Marekani miaka 13 iliyopita (September 11). Mazungumzo yao yalifanyika tarehe 11 Septemba 2014.
Mhe. Membe akimweleza jambo Balozi Childress wakati wa mazungumzo yao.
Balozi Childress pamoja na Bw. Vincent Spera, Afisa kutoka  Ubalozi wa Marekani wakimsikiliza Mhe. Membe (hayupo pichani)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. kuna vitu Watanzania huwa hatupendi kujifunza wala kuwasoma wenzetu... huwa hawa majamaa Wazungu , Wajapani hawapendi mambo ya kupeana mikono ila basi tuu...

    Halafu kinachowaudhi zaidi ila wanashindwa kusema kwasababu ni tamaduni zetu..Utakuta mwingine akisalimia anashika mkono halafu anaushek karibia dk 10 yeye ameshika mkono kisa kusalimia...Hawapendi.. Me kuna mmoja alishaniambia kuwa hapendi.

    Kingine pia ni tukumbuke mikono yetu wengine tuwapo makazini huwa tunashika vitu mbali mbali vitam tam kama zawadi vya kula na uwezekano wa kunawa kwa haraka hakuna maji karibu... Mikono mingine mtu anakuja kukung'angania kushika hujui yeye katoka wapi, kashika nini...Pengine amepanda daladala kashika chuma lile linashikwa na kila mmoja, pengine anaendesha gari usteling ule unashikwa na wengi, kashika viatu yaani bora tubadilikage..

    Na pia tukianza hivi hata tutakuwa tushaanza kujifunza kuepuka Ebola...

    ReplyDelete
  2. We anon wa kwanza with all due respect unakosea. There is a chance hujasoma business communication, umesahau tamaduni zinamata depending on the environment.

    Ukiwa Japan then u adhere to their traditions in some sense, likewise mgeni akija Tanzania its the same thing anatakiwa ajue sisi tunapendelea nini. Kwahiyo unataka mjapani akija kwetu sisi tuanze kuinama inama.. c'mon

    Kunawa mikono ni muhimu kila sehemu, and I am sure ofisi zetu TX zina vyoo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...