Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe Bernard K. Membe (Mb) (katikati) akikabidhi hundi yenye thamani ya Dola za Marekani laki moja kwa mtoto wa Brigedia Jen. Mstaafu Hashim Mbita, Bibi Shella Mbita. Bibi Mbita alipokea zawadi hiyo kwa niaba ya Baba yake ambayo imetolewa na Rais wa Zimbabwe, Mhe. Robert Mugabe kutokana mchango mkubwa alioutoa Brig. Jen. Mbita katika harakati za ukombozi Kusini mwa Afrika. Mwingine katika picha ni Balozi wa Zimbabwe nchini Tanzania, Mhe. Edzai Chimonyo.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu Tuzo iliyotolewa na Rais Mugabe kwa Brig. Jen. Hashim Mbita wakati wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa SADC uliofanyika Victoria Falls nchini Zimbabwe mwezi Agosti 2014. Waziri Membe alieleza kuwa Rais Mugabe alitoa Tuzo ya Munhumutapa kwa Brig. Jen Hashim Mbita kutokana na mchango wake mkubwa katika harakati za kutafuta uhuru Kusini mwa Afrika. Brig. Jen. Mbita anakuwa mtu wa kwanza sio Mkuu wa Nchi kutunukiwa Tuzo hiyo ambayo kwa kawaida hutukiwa Wakuu wa Nchi pekee. Wengine katika picha ni Balozi wa Zimbawe nchini Tanzania na binti yake Brig. Jen. Mbita, Bibi Shella. 
Bibi Shella akitoa neno la shukrani kwa Serikali ya Zimbabwe kutokana na zawadi ya Dola 100,000.00 kwa Baba yake mzazi
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Shiyo Innocent (tai nyekundu) na Afisa wa Ubalozi wa Zimbabwe nchini Tanzania wakifuatilia kwa makini mkutano wa waandishi wa habari
Waandishi wa habari wakiwa kazini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Zimbabwe imefanya vizuri kushukuru kwa kazi kubwa aliyoifanya Mzee Hashim Mbita.

    ReplyDelete
  2. Asante mzee mugabe

    ReplyDelete
  3. Imekuwa vyema kwa hiyo tuzo, lakini mwandishi hajawa wazi ni dola marekani au zimbabwe maana hata zimbabwe wanatumia dola

    ReplyDelete
  4. Anony wa 3 acha kukurupuka, kamilisha kusoma hiyo stori ili upate ufasaha wake1

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...