Mtoto Mwasiti Abdulrazack Kakurwa, miaka 14 (pichani), aliyetoweka nyumbani kwao Tandika, Wilaya ya Temeke, Mkoa wa Dar es salaam, mnamo tarehe 31/10/2014, katika mazingira ya kutatanisha, amepatikana jana.
Mwasiti ameletwa nyumbani kwa wazazi wake na bibi mmoja ombaomba anayesema kuwa binti huyo aliletwa maeneo ya kitumbini wanakolala ombaomba na Wanawake watatu Usiku na baadae wanawake hao wakatoweka katika mazingira ya ajabu!
 Baadae huyo bibi alimchukuwa Mwasiti na kukaa naye. Alipomuuliza huyo binti anatokea wapi, binti alisema hajui kwao ni wapi. Ila baadae huyo binti alipata ufahamu na kusema kwao ni tandika na kumuelekeza huyo bibi ni wapi wanapooishi wazazi wake. Asubuhi ya jana ndiyo bibi akamleta huyo binti nyumbani kwa wazazi wake.
Huyo bibi aliwekwa chini ya ulinzi wa polisi  na kuhojiwa sana. Na baada ya kujiridhisha na maelezo ya huyo bibi polise wameishauri familia kumuachia huyo bibi na familia imekubali aachiwe!
 Binti alipelekwa hospitali na kufanyiwa checkup na kuonekana yuko salama. 
Tunamshukuru Mola kwa kumrudisha salama binti yetu. Tunawashukuru watu wote waliokuwa karibu nasi wakati wote wa kuhangaika kumtafuta binti yetu.
Mimi Mubashiry Kakurwa, 
kwa niaba ya familia ya binti aliyekuwa amepotea.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. mazingaombwe matupu.

    ReplyDelete
  2. very strange, wakati mwingine ndo maana watu hawataki kusaidia.

    ReplyDelete
  3. Jamanj sii fahamu hii familia wala huyu binti, lakinj naona wasikae tu, hiyo hadithi ya kurudishwa na wanawake watstu......ina walakini. Akaombewe....... Kuna kitu hakipo sawa.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...