
“Ndugu rafiki na jamaa wa familia ya Pingapinga inakukumbusha kuwa
harusi ya mtoto wao imekaribia hivyo mchango wako unahitajika”, baada ya
wiki meseji huwa kali zaidi;“Siku zinaisha kwa nini hautoi mchango,
unajua familia ya Pingapinga ina shughuli ya harusi ya mtoto wao, toa
upesi au la usitulaumu.”
Basi hizi meseji zilikuwa nyingi kuliko zile za kampuni yangu ya simu
inayobuni namna ya kunitoa mkwanja kila wiki. Hatimaye nikatoa faini,
maana nisiite mchango, maana mchango haulazimishwi.
Sasa Jumamosi ndiyo ikawa siku ya harusi, kadi nililetewa mapema ,
nikahakikisha koti langu la kuendea harusini nalicheki vizuri, maana
haya makoti yanayokaa kabatini miezi ni muhimu kucheki vizuri maana
unaweza kukuta panya kazalia kwenye mfuko halafu wakatimka kutoka
kwenye makazi yao wakati uko katikati ya kucheza mduara wa harusi.
Kweli tukaingia ukumbini viti vilikuweko swafi, meza zimepambwa kwa maua na MC alitukaribisha kwa maneno mengi yaliyojaa vichekesho visivyochekesha, au vichekesho vingine vimesharudiwa na kila MC hapa mjini halafu akawa analazimisha watu wapige vigelegele! Yote bure watu walikuwa wamenuna maana hakukuwepo na dalili ya hata chupa moja ya kinywaji, ila ahadi kibao zikawa zinatolewa na MC, mara ‘Roli la bia linakuja toka breweries, mara shampeni leo inatoka Ufaransa kwa helikopta.”
Ghafla
wahudumu waliovalia vikofia kichwani wakapitisha sambusa
mojamoja kwa kila mtu, wakisindikizwa na MC akituhamasisha tule tufurahi
na bwana harusi. Kwa kweli hela yangu ikaanza kuniuma, kwanza
nililazimishwa kulipa, halafu sioni chochote hawa jamaa vipi? Wakati
ukumbi mzima ukiwa umeendelea kununa utadhani kikao cha msiba,
MC akatuambia eti bwana harusi ana machache kabla ya kutuaga kwenda
kupumzika na mkewe. Pamoja na kisirani tulikuwa na hamu kumsikia mshenzi
huyu anataka kusema nini.
Bwana harusi akasimama hata suti aliyovaa ilikuwa haijamkaa sawasawa,
akakohoa kidogo akaanza, “Asante MC, kwanza naomba nimshukuru Mungu kwa
kumuumba mke wangu, kwa hilo Mungu uko juu, kiukweli hapa nimepata mke
mtulivu, mpole asiye na makeke, yaani najisikia nina bahati sana.
“Naomba niwashukuru wakwe zangu kwa kukubali kupokea robo tu ya
mahari na kuruhusu ndoa hii ifanyike. Pia nishukuru kwa zawadi zao za
kitanda, godoro, kabati na makochi asante sana. Naomba nimshukuru baba
mwenye nyumba wangu kwa kukubali niwe na deni la kodi ya mwaka ili
kufanikisha harusi hii, mzee upo juu.
“Naomba nitoe shukrani kwa bosi wangu kwa kunipa likizo fupi ili
nikamilishe shughuli hii, pia wafanyakazi wenzangu kwa zawadi yenu ya
jiko la gesi. Namshukuru mke wa kaka yangu kwa kutuazima gauni la
harusi, na kaka yangu kwa suti hii niliyovaa. Natoa shukrani kwa
mtengeneza keki, nitairudisha keki kwako kesho kama tulivyokubaliana.
“Nawashukuru wazazi wangu kwa kuja na kikundi cha ngoma toka
kijijini, kweli kimeziba pengo la burudani katika harusi hii. Naishukuru
kamati ya wazee wa kanisa kwa kufanikisha kumshawishi mke wangu aolewe
na mimi, niwape aksante kwa akina mama jirani kwa kuja na sambusa
mlizokula toka makwao ili kufanikisha harusi hii, mradi harusi hii ni
furaha tupu. “MC wewe ni rafiki yangu nashukuru kwa kukubali tulipane
kidogokidogo aksante sanaaaaa
Safi sana, tena ningekuwa mimi hata sambusa nisingewapa, watu wanaacha kuchangiana mambo ya maana wanakomaa na michango ya harusi ifike wakati tubadilike michango ya harusi sio dili, leo Mzee kitime umetoa bonge la somo
ReplyDeletehahaha so funny!
ReplyDeleteAngeongezea kidogo na michango yenu tumeona si bora kukunulieni vinywaji kwani ajali nyingi husababishwa na unywaji wa pombe na kuendesha gari hivyo basi natoa tena shukran kwani michango yenu itatumika kununua kiwanja na kuacha mambo ya kupanga
ReplyDeleteMimi NIMEGOMA kuchangia harusi toka zamani za kale, kama ni kuchangia shule, magonjwa, kuomba mtaji basi nipo mstari wa mbele, cha kushangaza hakuna hata mmoja anayeniuliza nimmpige tafu kwa mambo ya maendeleo, ndugu jamaaa na marafiki wananijua kwa hilo ya kwamba sitoi michango ya harusi!
ReplyDeleteKuoa unaoa wewe,halafu "damage" niingie mimi?
Haswa michango imezidi eti kipaimara, graduation, birthday kama huna uwezo kaa kimya au fanya shughuli ndogo.
ReplyDelete