Shirika la DKT International limezindua rasmi kondomu mpya za Bull na Trust. Akizungumza katika uzinduzi huo, rais wa DKT ndugu Christopher Purdy alisema nia hasa ya kuleta bidhaa za kondomu nchini ni kusaidia katika jitihada za kukabiliana na uzazi wa mpango na pia magonjwa ya zinaa.

 Uzinduzi huo ulienda sambamba na usomaji wa ripoti ya utafiti wa tabia za kimapenzi kwa wakazi wa Dar es Salaam iliyofanywa na taasisi ya Data Vision International ambayo mojawapo ya matokeo ni ile iliyoonyesha idadi kubwa ya watu bado inashiriki mapenzi bila kutumia kinga.
Macmillan George toka Data Vision International akitoa ripoti ya tabia za kimapenzi kwa wakazi wa Dar es Salaam.
Wageni waalikwa wakifuatilia kwa umakini taarifa hiyo.
Rais wa DKT International Christopher Purdy akizungumza katika uzinduzi huo.
Meneja Masoko wa DKT International Davis Kambi akiongea kuhusu bidhaa hizo za kondomu.
Muonekano tofauti wa kondomu mpya za Bull.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Yenye vipele (studded) ndo ipi kati ya hizo?

    ReplyDelete
  2. It would have been fine if the logo was for boxing or mma gloves. It looks a bit too agressive for a condom. Mtu akiiangalia hiyo pembe asije "mjomba" akasinyaa!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...