Na Joseph Zablon, Kawe
Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa ameahidi kumsaidiana kwa maombi na njia zingine, Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima ili aweze kulipata eneo la Tanganyika Pakers analolitumia kwa mahubiri ili ajenge kanisa kwa ajili ya waumini wake.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa ameahidi kumsaidiana kwa maombi na njia zingine, Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima ili aweze kulipata eneo la Tanganyika Pakers analolitumia kwa mahubiri ili ajenge kanisa kwa ajili ya waumini wake.
Kauli ya Lowassa imefuatia ombi la askofu huyo wakati wa uzinduzi wa helkopta ya kanisa hilo ambayo ameahidi kuitumia kwa ajili ya kusaidia majanga yanapotokea na pia kusambaza neno la Mungu ambako alidai kuwa amesikia kuwa eneo hilo lipo katika mchakato wa kupatiwa mwekezaji.
“Nasikia hapa kuna mtu anataka kulinunua hili eneo hivyo naomba sana ikiwezekana liuziwe kanisa langu ili liweze kujenga kanisa kwa ajili ya waumini” alisema Gwajima wakati anamkaribisha waziri mkuu mstaafu kuzungumza katika hafla hiyo.
“Nasikia hapa kuna mtu anataka kulinunua hili eneo hivyo naomba sana ikiwezekana liuziwe kanisa langu ili liweze kujenga kanisa kwa ajili ya waumini” alisema Gwajima wakati anamkaribisha waziri mkuu mstaafu kuzungumza katika hafla hiyo.
Alisema Lowassa kuwa ombi na kilio hicho amekisia na anahidi kushirikiana nao kuhakikisha wanapata ardhi kwa ajili ya kanisa hilo
“Nitashirikiana nayi kwa maombi na njia zingine kuhakikisha mnapata ardhi kwa ajili ya kanisa hili” alisema.
Alibainisha kuwa Gwajima ni mmoja kati ya viongozi wenye maono ambao kimsingi ndio wanaohitajika kwa ajili ya ustawi wa jamii.
Awali Askofu Gwajima alisema kuwa helkopta hiyo ni moja kati ya zingine mbili zinazotarajiwa mwakani kwa ajili ya huduma za kanisa na uokozi.
Alisema kuwa ameshawishika kuinunua baada ya kuona abiria waliokuwa katika meli yam v Spice walivyopoteza maisha kutokana na kukosa msaada hali ambayo inawapata pia majeruhi wa ajali zingine ambao wengi hufariki dunia wakiwa njiani kukimbizwa hospitalini.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiwasili viwanja vya Tanganyika Packers,Kawe jijini Dar es salaam kwa ajili ya uzinduzi wa helkopta ya
Kanisa la Ufufuo na Uzima la Askofu Josephat Gwajima jijini Dar es Salaam jana.Picha zote na Othman Michuzi.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akizungumza kabla ya uzinduzi huo.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Helkopta ya Mchungaji Josephat Gwajima wa Kanisa la Ufufuo na Uzima (kulia kwa Mh. Lowassa).
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiikagua helkopta hiyo mara baada ya uzinduzi.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiteta jambo na rubani wa Helkopta hiyo muda mfupi baada ya kuizindua.
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
Waumini wakishuhudia uzinduzi wa helkopta hiyo
BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI
Really! This is a comedy! Eneo hilo lifanywe la shughuli yeyote ile ya maendeleo ama biashara sio kanisa. Lets be serious.
ReplyDeleteKwa upande mwingine, Kanisa linawasaidia vipi watu kwa helikopta? Itolewe basi kwa Jeshi la Polisi ama traffic polisi ambao ndio wa kwanza kupata taarifa za maaafa!! How this works for the Church other than egos raises a lot of questions!!
Kiwanja cha Tanganikia Packers ni mali ya umma na kuna utaratibu unaotakiwa kufuatwa ili kupata mali kama hiyo.
ReplyDelete