Na Joseph Zablon, Kawe Dar es Salaam.

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa ameahidi kumsaidiana kwa maombi na njia zingine, Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima ili aweze kulipata eneo la Tanganyika Pakers analolitumia kwa mahubiri ili ajenge kanisa kwa ajili ya waumini wake. 

Kauli ya Lowassa imefuatia ombi la askofu huyo wakati wa uzinduzi wa helkopta ya kanisa hilo ambayo ameahidi kuitumia kwa ajili ya kusaidia majanga yanapotokea na pia kusambaza neno la Mungu ambako alidai kuwa amesikia kuwa eneo hilo lipo katika mchakato wa kupatiwa mwekezaji. 

“Nasikia hapa kuna mtu anataka kulinunua hili eneo hivyo naomba sana ikiwezekana liuziwe kanisa langu ili liweze kujenga kanisa kwa ajili ya waumini” alisema Gwajima wakati anamkaribisha waziri mkuu mstaafu kuzungumza katika hafla hiyo. 

Alisema Lowassa kuwa ombi na kilio hicho amekisia na anahidi kushirikiana nao kuhakikisha wanapata ardhi kwa ajili ya kanisa hilo 
“Nitashirikiana nayi kwa maombi na njia zingine kuhakikisha mnapata ardhi kwa ajili ya kanisa hili” alisema. 

Alibainisha kuwa Gwajima ni mmoja kati ya viongozi wenye maono ambao kimsingi ndio wanaohitajika kwa ajili ya ustawi wa jamii.

Awali  Askofu Gwajima alisema kuwa helkopta hiyo ni moja kati ya zingine mbili zinazotarajiwa mwakani kwa ajili ya huduma za kanisa na uokozi. 
Alisema kuwa ameshawishika kuinunua baada ya kuona abiria waliokuwa katika meli yam v Spice walivyopoteza maisha kutokana na kukosa msaada hali ambayo inawapata pia majeruhi wa ajali zingine ambao wengi hufariki dunia wakiwa njiani kukimbizwa hospitalini.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa  akiwasili viwanja vya Tanganyika Packers,Kawe jijini Dar es salaam  kwa ajili ya uzinduzi wa helkopta ya Kanisa la Ufufuo na Uzima la Askofu Josephat Gwajima  jijini Dar es Salaam jana.Picha zote na Othman Michuzi.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa  akizungumza kabla ya uzinduzi huo.

Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Helkopta ya Mchungaji Josephat Gwajima wa Kanisa la Ufufuo na Uzima (kulia kwa Mh. Lowassa).
 Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa  akiikagua helkopta hiyo mara baada ya uzinduzi.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa  akiteta jambo na rubani wa Helkopta hiyo muda mfupi baada ya kuizindua.

Waumini wakishuhudia uzinduzi wa  helkopta hiyo 

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Really! This is a comedy! Eneo hilo lifanywe la shughuli yeyote ile ya maendeleo ama biashara sio kanisa. Lets be serious.

    Kwa upande mwingine, Kanisa linawasaidia vipi watu kwa helikopta? Itolewe basi kwa Jeshi la Polisi ama traffic polisi ambao ndio wa kwanza kupata taarifa za maaafa!! How this works for the Church other than egos raises a lot of questions!!

    ReplyDelete
  2. Kiwanja cha Tanganikia Packers ni mali ya umma na kuna utaratibu unaotakiwa kufuatwa ili kupata mali kama hiyo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...