Rais wa Taasisi ya kijamii ya Wanawake wenye Mafanikio Tanzania (Tanzania Women of Achievement ),Bi. Irene Kiwia (kulia) akisisitiza jambo mbele ya wanahabari (hawapo pichani) juu ya utoaji wa Tuzo za Wanawake wenye Mafanikio Tanzania ambazo zitafanyika Machi 7,2015 kwa mara ya nne tangu kuanzishwa kwake, ikiwa na lengo la kuwatambua na kuwapongeza wanawake ambao wamechangia maendeleo ya nchi katika nyanja tofauti.Wengine pichani ni Mwenyekiti wa Tuzo za Wanawake wenye Mafanikio Tanzania (TWAA), Mama Sadaka Gandhi (katikati) na kushoto ni Katibu Mkuu wa Tuzo za Wanawake wenye Mafanikio Tanzania (TWAA),Bi. Hellen Kiwia.
Mwenyekiti wa Tuzo za Wanawake wenye Mafanikio Tanzania (TWAA), Mama Sadaka Gandhi (katikati) akitoa ufafanuzi juu ya namna Tuzo hizo zitakavyokuwa zikitolewa na wanaohusika kupewa tuzo hizo,wakati wa mkutano na wanahabari (hawapo pichani) uliofanyika leo kwenye Ukumbi wa Hoteli ya Serena,Jijini Dar es Salaam.Kulia ni Rais wa Taasisi ya kijamii ya Wanawake wenye Mafanikio Tanzania (Tanzania Women of Achievement ),Bi. Irene Kiwia na kushoto ni Katibu Mkuu wa Tuzo za Wanawake wenye Mafanikio Tanzania (TWAA),Bi. Hellen Kiwia.
Katibu Mkuu wa Tuzo za Wanawake wenye Mafanikio Tanzania (TWAA),Bi. Hellen Kiwia akielezea namna ya wanawake watakavyoshiriki ili kuweza kupata Tuzo hizo.
Sehemu ya Waandishi wa habari waliohudhulia Mkutano huo.
Timu nzima ya Taasisi ya kijamii ya TWA (Tanzania Women of Achievement ) inayoratibu utoaji wa tuzo za Wanawake wenye Mafanikio Tanzania (TWAA) wakiwa kwenye picha ya pamoja.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Kipimo cha Mafanikio ni kipi? Elimu, mali, madaraka, utunzaji wa familia au nini?

    ReplyDelete
  2. Hawa kiwia wawili ni ndugu? Helen kama huna mtu basi tutafutane.

    ReplyDelete
  3. kipimo cha mafanikio ni kumcha MUNGU katika roho na wali siyo rasilimali (elimu, madaraka, mali, etc...)

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...