Dereva Toka Nchini Ujerumani Rainer Zietlof akiwa na Meneja mkuu wa Alliance Autos Bwana Wayne Mcintosh(wa pili toka kulia)wakipata picha ya pamoja na wanahabari
Meneja Mkuu wa Alliance Autos Wayne Mcintosh(kushoto) Akipata picha na Dereva Toka Nchini Ujerumani Rainer Zietlof
Meneja Masoko wa Alliance Autos Tharaia Ahmed(kushoto)akipata picha na Dereva Rainer Zietlof
Meneja mkuu wa Alliance Autos Bwana Wayne Mcintosh akisoma cheti cha rekodi ya dunia alichopewa dereva toka ujerumani
-----------------------------------------
DEREVA raia wa Ujerumani Rainer Zietlof yuko mbioni kuvunja rekodi ya dunia ya kuendesha gari kwa kilometa 17,000 kutoka Ulaya hadi Afrika.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Zietlof alisema kuwa hiyo itakuwa ni rekodi yake ya tatu baada ya zile za awali alizovunja mwaka 2011 na 2012.
Awali alivunja rekodi baada ya safari iliyojulikana kama 'Panamerica'ambayo ilimchukua kutoka Tierra del Fuego hadi Alaska kwa siku 11 na saa 17 wakati ile ya 'Russtralia' ilimtoa Melbourne, Australia hadi St.Petersburg nchini Urusi ambako alitumia saa 18.
Zietlof anayetumia gari aina ya VW Touareg V6 TDI alianza rasmi safari yake Septemba 21 mwaka huu huko North Cape nchini Norway na anatarajia kuikamilisha nchini Afrika Kusini, ambako atakuwa ametembea kwa kilometa 17,000.
Kwa mujibu wa dereva huyo, safari hiyo ndefu imempitisha katika nchi za Norway, Finland, Sweden, Denmark, Ujerumani, Jamhuri ya Czech, Slovakia, Hungary, Serbia, Bulgaria, Uturuki, Misri, Sudan, Ethiopia, Kenya na sasa Tanzania.
Dereva huyo alizungumza na wandishi wa habari katika makao makuu ya Alliance Autos iliyopo barabara ya Nyerere jijini Dar es Salaam, na kusema kuwa atachangia kiasi cha senti 20 za euro kwa kila kilomita, kwa vijiji nchini Tanzania na Zambia.
Mbali na kuahidi kuvichangia vijiji hivyo, Zietlot pia amesisitiza kuvitembelea vijiji hivyo atakavyo vichangia.
Aidha, amelisifia gari hilo kutokana na uwezo wake wa kukabiliana na mazingira tofauti tofauti ya hali ya hewa kama baridi kali na joto pamoja na barabara mbovu.
Mradi huu wa kuzunguka sehemu mbalimbali za dunia kwa gari hilo umedhaminiwa na makampuni makubwa ya magari ya Tehama na Volkswagen nchini Ujerumani, Slovakia na Afrika Kusini.
Katika safari hiyo Zietlow yuko na wasaidizi wake wawili, Marius Biela ambaye ni mpiga picha na mchukua video huku Matthias Prillwitz ni mzoefu wa mbio
za magari nchini Ujerumani.
Dereva huyo alianza safari zake za barabarani mwaka 2005 na ameoa na ana mtoto mmoja. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...