Maofisa wa Uhamiaji kutoka Dar Es Salaam na Zanzibar wameanza zoezi la kupokea maombi ya pasipoti kutoka kwa Watanzania waliopo nchini Italy. Maofisa hao wanategemewa kuelekea katika nchi za Turkey na Greece,kwa ajili ya zoezi hilo hilo.

 Haya ni matunda ya Kamati ya Diaspora iliyokutana na Mh Balozi James Alex Msekela, mwezi juni mwaka huu. Kamati ilikutana na balozi na maofisa wa juu wa kibalozi kwa ajili ya kutambulisha kamati na uongozi wake,na pia kuwakilisha kero na matatizo ya watanzania wanaoishi Italy . 

Mkutano huo uliisha kwa mafanikio makubwa. Kwa hiyo haya ni matokeo ya uchapa kazi wa kweli wa mh Balozi Dkt James Alex Msekela, kwani katika mapumziko yake nchini Tanzania mwezi August mwaka huu alitumia muda wake kukutana na Kamishna wa Uhamiaji Tanzania kujadili suala la matatizo ya Pasipoti kwa watanzania wa Maeneo ya uwakilishi wake.
Baadhi ya Maofisa wa Uhamiaji ambao wako nchini Italy hivi sasa,wakiendelea na kazi rasmi ya  kutatua matatizo ya pasipoti kwa watanzania waishio nchini humo, wakiwa katika siku ya pili ya zoezi hilo,ambalo linaanzia asubuhi mapema saa 3 hadi saa kumi na mbili jioni.
Afisa Uhamiaji akichukua maelezo ya mmoja wa Watanzania waishio nchini Italy wakati wa zoezi la kutatua matatizo ya pasipoti kwa watanzania hao.

Sehemu ya Watanzania hao wakisubiri kutatuliwa matatizo yao ya pasipoti.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. kwa hiyo wanapewa passport za tanzania na wakati huo huo wanazo za Italy wanazo kibindoni? iko wapi ile sheria ya kukataza uraia wa nchi mbili?

    ReplyDelete
  2. hamna kaka hawa hawana hata karanga mundu, yani kitamburisho chochote wanaishi tu ovyo ovyo, Italy si mchezo mbuzi karamba reli

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...