Shirika la Ndege
la Taifa la Shelisheli, Air Seychelles limeanza kufanya safari zake kati ya mji
mkuu wa nchi hiyo, Mahe na Dar es Salaam ambapo Desemba 2, 2014, ndege
yake ya abiria HM 777 ilifanya safari yake ya kwanza ya uzinduzi kwa kutua Kiwanja
cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam.
Ujio wa shirika
hilo la ndege unafanya mashirika ya ndege yaliyoanzisha safari zake kuja Dar es
Salaam kwa siku za hivi karibuni kufikia matatu, Air Seychelles, Flydubai ya
Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) na Rwandair ya Rwanda. Shirika lingine la ndege,
Etihad la Abudhabi (UAE) linatarajiwa kuanza safari zake mwaka 2015.
Ndege ya abiria HM 777 Ya Airseychelles baada ya safari yake ya kwanza ya uzinduzi kwa kutua Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam.
Tunaomba hili shirika liongeze safari pia za Dar - Comoro maana wasafiri wa rout hiyo tunapata dhiki sana na ndege zetu za Air Tanzania na Precission
ReplyDeleteSasa kwenda Shelisheli itakuwa kama kwenda Tabora vile:-)
ReplyDelete