Shirika la Ndege la Taifa la Shelisheli, Air Seychelles limeanza kufanya safari zake kati ya mji mkuu wa nchi hiyo, Mahe na Dar es Salaam ambapo  Desemba 2, 2014, ndege yake ya abiria HM 777 ilifanya safari yake ya kwanza ya uzinduzi kwa kutua Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam.


Ujio wa shirika hilo la ndege unafanya mashirika ya ndege yaliyoanzisha safari zake kuja Dar es Salaam kwa siku za hivi karibuni kufikia matatu, Air Seychelles, Flydubai ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) na Rwandair ya Rwanda. Shirika lingine la ndege, Etihad la Abudhabi (UAE) linatarajiwa kuanza safari zake mwaka 2015.
Ndege ya abiria HM 777  Ya Airseychelles baada ya  safari yake ya kwanza ya uzinduzi kwa kutua Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Tunaomba hili shirika liongeze safari pia za Dar - Comoro maana wasafiri wa rout hiyo tunapata dhiki sana na ndege zetu za Air Tanzania na Precission

    ReplyDelete
  2. Sasa kwenda Shelisheli itakuwa kama kwenda Tabora vile:-)

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...