Katika pita pita za kila siku mtaani,hivi karibuni kamera yetu ilikatiza maeneo ya Vingunguti pembezoni mwa bonde la Mto Msimbazi na kukutana na hali kama ionyekanavyo pichani hapa.kiukweli mambo si shwari katika eneo hili hasa usalama wa afya kwa wakazi waliozunguka eneo hilo.ukiangalia kwa makini utabaini kuwa kuna watoto wadogo wakiendelea na michezo katika eneo hilo bila kufahamu kuwa wapo hatarini kiafya.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Hili bonde ni chafu, hivi kuna wahusika, kama wapo wanafanya nini?

    ReplyDelete
  2. Natamani Meya aione. Duh sijui mwendo huu mpaka lini?

    ReplyDelete
  3. Watanzania mnachekesha hilo dampo lipo ni sehemu ya watu na ndo maana Hawaathiki immune system Yao inatisha . Hapo limeshaanza Kuwa uzunguni Masaki kwani natamani ungeliona likiwa bado wanamwaga taka hapo watu walikuwa wanaokota kila kitu Hadi chakula na kulikuwa na depot za matycoon wa kuuza bidhaa zinazotoka hapo eti mnatamani mafisadi walione kwani Nani halIjui hilo dampo kwa kifupi tu watu wa maeneo hayo ni zaidi ya Wanyama Kwa sugu ya immune system

    ReplyDelete
  4. Msomaji hapo juu unashangaa? Ama unaishi nje ya nchi? Hapa mtaani kwangu kwenye eneo la maduka na kituo cha daladala, kuna kiwanja hakijajengwa. Sasa hapa kwenye hiki kiwanja kwa miaka mingi pamekua ni mahali pa kutupa takataka za kila aina - kuku waliokufa, mbwa waliokufa, manyoya ya kuku kutoka kwa wafugaji, n.k., n.k. Huu ni mfano mmoja tu. Ukiwa Dar tafuta muda uzunguke mitaani hasa kwa waswahili wa kawaida ujionee. Ukweli ni kwamba hata sisi wananchi hasa wa Dar tumeshazoea mazingira ya uchafu na tunaona ni kawaida tu. It is very sad.

    ReplyDelete
  5. Kila tatizo utakaloliona Tanzania chanzo chake ni rushwa na ufisadi. Barabara mbovu, uchafu, tatizo la maji, elimu kudorora, huduma za afya mbovu, nk, nk.

    Kinachotokea ni kwamba, ile pesa yote ambayo ingekwenda kutatua haya matatizo ndiyo inayokwenda kwa wala rushwa na mafisadi. Kwa hiyo watanzania wenzangu, kila unapokula rushwa au unapochukua fungu la kifisadi ujue unaiumiza jamii ikiwa ni pamoja na kujiumiza wewe mwenyewe.

    Mimi mwenyewe sio mtakatifu. Juzi tu nimepokea fungu, lakini kwa matendo yangu serikali imepoteza mara kumi ya fungu nililochukua. Roho yangu inanishtaki, lakini nikiacha kuchukua mwingine atachukua. Yaani hapo ndipo hii nchi yetu ilipofika.

    Mheshimiwa raisi, nakuomba ufanye kile serikali ya China inachofanya. Weka jela wala rushwa na mafisadi bila kujali cheo au wadhifa wa mtu.

    Mimi sipendi rushwa, lakini wote tunaogelea kwenye bahari ya rushwa. Tunalazimika kunywa maji ya rushwa. Tunahitaji mikakati ya maksudi ya kujinasua tulipofika na ninaamini mheshimiwa raisi kwa ujasiru wako unaweza.

    ReplyDelete
  6. hayo maeneo mngemuelekeza huyu Mzee wa Mtaa kwa Mtaa akatuletee taswira zake tuzione.Halafu huyu jamaa wa Mtaa kwa Mtaa namuaminia sana katika sekta hii.sijui alikumbwa na nini akapoteza Dira?? ila sasa naona karudi kwa speed ya ajabu. Hongera sana kwake.

    Ankal kijana yuko vizuri sana......

    ReplyDelete
  7. Hivi hilo eneo tunaweza re-claim? Naona kama pamekaa vizuri kwa biashara... Watu hawajalishtukia kama dampo la tabata? Magereji ya kufa mtu.... Hapo jirani na mto ka-pub au ukumbi wa starehe inawezekana... Meya wa Ilala tunaomba audience

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...