
Mwimbaji
huyo anasema kuwa amejipanga vilivyo ikiwa pamoja na kufanya maandalizi
ya hali ya juu huku akisistiza kuwa atafanya makubwa katika tamasha la
Krismasi ambalo litakuwa la pili kufanyika.
Mwaipaja
anasema kuwa anawaomba mashabiki wafike kwa wingi kwa sababu amepewa
nafasi hiyo ya kulihubiri neno la Mungu kupitia uimbaji hivyo yupo kwa
ajili yao ni vema wakajitokeza kwa wingi kupata upako.
“Naimba
kwa ajili ya kumtumikia Mungu, natoa huduma kwa njia ya uimbaji hivyo
watanzania wajitokeze siku hiyo muhimu ya kuzaliwa kwa Yesu naamini
watafurahi kwa jinsi ninavyofanya maandalizi ya tamasha hili kubwa
ambalo limepangwa kufanyika siku yenye Baraka za Mungu,”
Mwimbaji
huyo anayevuma na nyimbo zake nyingi ambazo anatarajia kuziimba katika
tamasha hilo la aina yake aliziita atakazoimba kuwa ni pamoja na
Tusikate ‘Tamaa’ ambako alisema kuwa anaupenda wimbo huo kwa sababu
wengi unawatia moyo.
Anasema
kuwa mbali ya wimbo huo ambao upo kwenye albamu yake ya kwanza pia
anatarajia kuimba wimbo wa ‘Ombi langu’ambao unapatikana katika albamu
yake ya pili huku akifafanua kuwa maana ya wimbo huo kuwa mungu
ametengeneza njia katikati ya aliowakumbuka nay eye yumo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...