
WaziriMkuu,
MizengoPinda akisalimiana na Mbunifu wa kimataifa wa Mavazi, Sheria
Ngowi alipotembelewa jana nyumbani kwake Masaki jijini Dar esSalaam.
(Picha Zote: AtuzaNkurlu-SheriaNgowi Brand).
Mbunifu
wa kimataifa wa Mavazi, Sheria Ngowi akimuonesha Waziri Mkuu, Mizengo
Pinda baadhi ya vitambaa vya kisasa vya suti ambavyo vitatuka
Kumtengenezea Waziri Mkuu jana jijini Dar es Salaam.
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akiangalia na kuchagua aina ya vitambaa vya suti
amabvyo vitatumika kutengenza baadhi ya Suti Zake alipotembelewa na
Mbunifu wa Kimataifa wa Mavazi, Sheria Ngowi jana jijini Dar es
Salaam.(Picha Zote: Atuza Nkurlu-Sheria Ngowi Brand).
Tuwaunge mkono madesigner waki Tanzania.
ReplyDeleteAnkal, nimeguswa sana na taarifa hii. Mheshimiwa Pinda ameonyesha mfano mzuri kwa kumtambua na kumtumia mbunifu wa mavazi m-Tanzania, wakati wengine wanaenda kununua ughaibuni.
ReplyDeleteTunao wataalam wananchi katika fani mbali mbali, kuanzia ubunifu wa mavazi, kama hivyo, hadi upishi, kama tunavyoshuhudia kwa Chef Issa ambaye ni mshindi wa kimataifa. Watu wenye wadhifa katika jamii wakiwa na tabia ya kuwaenzi hao wananchi kama anavyofanya Mheshimiwa Pinda, manufaa yake ni makubwa. Itatusaidia kujenga utamaduni tofauti na huu ulioota mizizi wa kushabikia mambo ya ughaibuni, na itasaidia kuboresha uchumi wetu.