MTU mmoja anayekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 27 mpaka 30, ambaye jina lake halikufahamika mara moja,amekutwa akining'inia juu ya mti wa Mwembe uliopo katikati ya pori, nje kidogo ya mji wa Pongwe,Mkoani Tanga akidhaniwa kuwa amejinyonga.

Hali ya sintofahamu iliendelea kutanda katika eneo hilo huku kila aliefika eneo hilo la tukio,alijikuta akipigwana butwaa na kustaajabu ya kuwa ni kipi kilichomsibu kijana yule wa makamo mpaka kufikwa na mauti ya aina ile.

Akizungumza mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo, kwa sharti la kutotaja jina lake,alieleza kuwa ,walipata taarifa za tukio hilo kutoka kwa kijana mmoja aliekuwa akichunga ng'ombe katika pori hilo, ambaye pia jina lake halikufahamika mara moja,hali iliyowapelekea kwenda moja kwa moja eneo la tukio kushuhudia na kuona kama watamtambua mtu huyo ama la,lakini kila aliefika kwenye tukio hilo,hakuweza kumtambua huku wengine wakisema huenda mtuu huyo alikuwa ni mgeni kijijini hapo.

Ripota wetu aliyepo Jijini Tanga anaendele na juhudi za kumtafuta Kamanda wa Polisi wa Mkoa huo ili kuona kama anataarifa zozote juu ya tukio hilo.
Sehemu ya Wananchi wakazi wa Mji wa Pongwe Mkoani Tanga wakiangalia mwili wa mtu huyo uliokuwa ukining'inia juu ya mti.Ambapo mpaka ripota wetu anaondoka eneo la tukio hakukuwa na Mwanausalama yeyote aliefika eneo hilo.
Safari ya kuingia kwenye pori hilo kwenda kushuhudia na kuona kama watamtambua mtu huyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...