Mkurugenzi wa Operesheni wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Asumpta Malya, akionyesha tuzo ambayo PPF ilipata kwenye shindano la Afrika linaloandaliwa na taasisi ya ISSA, kuhusu utoajin bora wa huduma wa mifuko ya hifadhi ya jamii barani Afrika, hususan kwenye fao la elimu. Alikuwa akiwaonyesha wahariri wa vyombo vya habari kwenye semina ya siku moja iliyoandaliwa na Mfuko huo mjini Bagamoyo, mkoa wa Pwani Jumamlosi Desemba 13, 2014 baada ya kuibuka mshindi wa kwanza kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii kwa utoaji huduma bora kwa wanachama wake.Alikuwa akiwaonyesha wahariri wa vyombo vya habari kwenye semina ya siku moja ya Wahariri wa vyombo vya habari iliyofanyika mjini Bagamoyo , mkoa wa Pwani, Jumamosi Desemba 13, 2014.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio, akitoa hotuba ya ufunguzi wa semina ya siku moja ya wahariri wa vyombo vya habari nchini, iliyofanyika Jumamosi Desemba 13, 2014, huko Bagamoyo mmkoani Pwani.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...